Kauli ya Hassan Kabunda baada ya Kusikia Yanga na Simba zinamwitaji

Kauli ya Hassan Kabunda baada ya Kusikia Yanga na Simba zinamwitaji

0

Kauli ya Hassan Kabunda baada ya Kusikia Yanga na Simba zinamwitaji

Moja kati ya Mawinga ambao walikuwa machachari sana kwa misimu miwili iliyopita na mwanzoni mwa msimu kabla ya Kuwa majeruhi kwa muda na Kisha Kurejea Hassan Kabunda ametoa neno baada ya taarifa kuenea kuwa vigogo Simba na Yanga wote kuwa katika mahitaji naye.

Kabunda ambaye kwasasa anakipiga katika klabu ya Mwadui Fc kuna tetesi kuwa Yanga na Simba zote za Dar Es Salaam zinamwitaji huku Simba ikianza kutajwa hivyo toka kipindi cha Dirisha dogo.

Kabunda ambaye aliwahi kuitwa mpaka timu ya Taifa ya Tanzania amefunguka kuwa yeye yupo tayari kucheza timu yoyote ambayo itakaa naye mezani na kuelewana.

Urahisi zaidi kwa Timu inayomuhitaji Kabunda ni kwamba anamaliza mkataba wake na Mwadui Msimu Huu.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY