Kwa haya matatu lazima Yanga wachekelee leo kwa Mbao Fc

Kwa haya matatu lazima Yanga wachekelee leo kwa Mbao Fc

0

Kwa haya matatu lazima Yanga wachekelee leo kwa Mbao Fc

Mabingwa wa Kihistoria wa Tanzania klabu ya Yanga leo itashuka dimbani uwanja wa Taifa Kuvaana na Mbao Fc katika Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara VPL.

Kuelekea Pambano hilo Yanga anarekodi mbaya zaidi kwa Mbao Fc pengine kuliko timu yoyote ile inayoshiriki ligi Kuu kwani katika mechi 4 walizocheza Yanga ameshinda mechi 1 tu huku akipoteza mechi 3 kwa mbao Fc.

Tetesi za usajili Yanga 21 May 2018

Yanga Itakuwa ikichekelea mambo matatu kuelekea mchezo Huo jambo la Kwanza ni Mbao kumkosa Kinara wao wa Mabao lakini pia Muuaji wao msimu uliopita na msimu Huu pia Habib Haji Kiyombo.

Kiyombo yupo kwenye Msafara wa Ngorongoro Heroes iliyoenda Mali, Lakini Jambo jingine ambalo Yanga inaweza ikawa inachekelea kuelekea mchezo huo ni Kukosekana kocha aliyeitesa zaidi Yanga kila ilipocheza na Mbao Fc kocha Ettiene ambaye ameachana na Mbao Fc.

Zahera hajaridhishwa na Mchezaji Huyu Yanga

Jambo la tatu ni Mbao kutokuwa kwenye hatari ya Kushuka daraja tena, Kama hii mechi Mbao angekuwa bado kwenye hatihati ya Kushuka daraja basi ingekuwa Ngumu zaidi ya Ambavyo inaenda kuwa Leo.

Tusubiri dakika 90 Ziweze Kuamua pambano hilo ambalo Kwataunit Tutakuletea Moja kwa Moja baadae.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY