Lechantre ataja watano waliomkosha zaidi Simba toka atue,Asema wanaweza kucheza Nje

Lechantre ataja watano waliomkosha zaidi Simba toka atue,Asema wanaweza kucheza Nje

0

Lechantre ataja watano waliomkosha zaidi Simba toka atue,Asema wanaweza kucheza Nje

MABINGWA wa Ligi Kuu Bara msimu huu, Simba wamefanya usajili wa nyota 12 katika dirisha kubwa na nyota mmoja Asante Kwasi kutoka Lipuli katika dirisha dogo, lakini ni watano tu waliomkosha kocha Mfaransa, Pierre Lechantre.

Lechantre alisema katika kikosi chake tangu ametua hapa nchini miezi mitano iliyopita, amebaini kuwa usajili mkubwa uliofanywa na uongozi ulikuwa mzuri kuliko timu yoyote hapa nchini.

Kocha huyo aliyewahi kumnoa mchezaji bora mara nne Afrika, Samuel Et’oo, alisema alikuta timu ipo katika hali nzuri na wachezaji wazuri ila kulikuwa na vitu vidogo ambavyo aliviongezea na timu kuweza kuimarika zaidi.

Wachezaji ambao wamemkosha zaidi Mfaransa huyo ni Shomary Kapombe, Aishi Manula, Emmanuel Okwi, John Bocco na Erasto Nyoni na kuweka wazi kuwa, wamekuwa na msaada kufanikisha timu kubeba ubingwa, lakini wasingeweza kufanya hivyo bila kushirikiana na wenzao.

“Wachezaji wote wapo vizuri lakini kwa hao wanastahili pongezi kwa kila mmoja kwa nafasi yake alivyocheza pia yupo Jonas Mkude alikuwa vizuri ingawa muda mwingine alikuwa ananikera. Ana uvivu fulani,” alisema.

“Nimefundisha soka nchini nyingi na kwa viwango vya Kapombe, Manula, Mkude, Bocco, Okwi na Nyoni wanaweza kucheza soka hata Ufaransa.

Source : Mwanaspoti

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY