Makala : Jicho la Lwandamina halikuwa sawa kwa Matheo Antony

Makala : Jicho la Lwandamina halikuwa sawa kwa Matheo Antony

0

Makala : Jicho la Lwandamina halikuwa sawa kwa Matheo Antony

Kuna msemo huwa unasema Kila Nabii na zama zake, Kama msimu huu ungeisha Yanga ikiwa na aliyekuwa kocha wake George Lwandamina bila shaka katika orodha ya wachezaji ambao angewaacha jina la Matheo Anthony angeliorodhesha.

Ni jina ambalo ungeweza Kusema lilisahaulika kabisa ndani ya Yanga huku baadhi ya washabiki wakifikiri labda Matheo Anthony aliachwa na Yanga na Wengine wakifikiri labda ni Mgonjwa na Mambo kama Hayo.

Hakupata nafasi kabisa kwenye Kikosi cha Mwalimu George Lwandamina kuanza na hata kuwa kama Mchezaji wa Akiba kwenye Kikosi cha Yanga msimu Huu.

Matheo Anthony kwa msimu huu alianza Kuonekana katika Mchezo kati ya Tanzania Prisons dhidi ya Yanga baada ya Kikosi cha Yanga kugawanyika mara mbili.

Katika mchezo huo alionekana kuwa si mbaya sana, Akaja kuonekana pia katika kikosi cha Yanga akicheza dhidi ya Mtibwa kule Morogoro akazidi kuonekana kuwa anakitu kizuri tu kwenye Miguu yake.

Lakini katika mchezo kati ya Yanga dhidi ya Mbao Fc akiingia Kipindi cha Pili kuchukua nafasi ya Yusuph Mhilu Matheo Anthony alibadili mawazo ya watu wengi sana juu ya uwezo wake.

Usingedhani Kama Matheo Anthony ni mchezaji wa Kuwekwa Benchi kiasi cha Kukumbukwa mwishoni mwa msimu tena Kikosi kikiwa kwenye majanga ndipo akumbukwe.

Katika mchezo dhidi ya Mbao Fc Matheo akiingia dakika ya 47 alifanikiwa Kupiga mashuti matano Langoni mawili yakichezwa na Kipa na Moja kugonga Mwamba huku akitoa assists kadhaa ambazo zilishindwa kutumiwa Vizuri ikiwemo moja ya wazi aliyompigia Geofrey Mwashiuya.

Yanga Kucheza na Ruvu Shooting leo

Kucheza kwa kasi, kujiamini ,Uwezo wa Kumiliki Mpira lakini Pia kupiga langoni kulifanya washabiki wachache wa Yanga waliofika uwanja wa Taifa kumshangilia kwa Nguvu Matheo Anthony.

Swali la Kujiuliza msomaji wa Kwataunit  ni Kwa Lwandamina ambaye katika list ya Wachezaji waliowasilishwa CAF kwaajili ya Mashindano ya Kimataifa Matheo Anthony hakuwemo kabisa.

Na Hata wakati Yanga ikisota kuwakosa washambuliaji wake kama Amis Tambwe, Donald Ngoma na wengineo wenye asili hiyo alikuwa analazimika kuwatumia baadhi ya wachezaji ambao siyo wenye asili ya Kucheza kama Washambuliaji.

Kama hakukuwa na Tatizo kati ya Lwandamina na Matheo Anthony basi ni wazi Jicho la Lwandamina halikuwa sawa kwenye uwezo wa Matheo Anthony.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY