Matokeo Real Madrid vs Liverpool 26 May 2018

Matokeo Real Madrid vs Liverpool 26 May 2018

0

Matokeo Real Madrid vs Liverpool 26 May 2018

Matokeo Fainali ya UEFA champions League Real Madrid vs Liverpool 26 May 2018, Kwataunit.com Tutakupa Matokeo ya Moja Kwa Moja msomaji wetu ambaye hujapata nafasi ya Kuangalia Live kideoni.

Mechi imeanza

Real Madrid 0 – 0 Liverpool

Dakika ya Pili Madrid wanajaribu kutengeneza shambulizi lakini tayari ni Offside

Dakika ya 3 Liverpool wanajaribu kufika langoni mwa Madrid lakini mabeki wa Madrid wanakuwa Kizingiti

Dakika 5

Real Madrid 0 – 0 Liverpool

Dakika 7 Liverpool wanaonekana kucheza vizuri zaidi wakilisakama lango la Real Madrid katika dakika za Mwanzo

Dakika ya 10 Marcelo anajaribu shuti nje ya 18 Mpira Unakwenda Nje

Dakika ya 15 Ronaldo anajaribu kuingia kwa Kasi anapiga Mpira Unapaa Juu ya Lango

Dakika 15

Reald Madrid 0 – 0 Liverpool

Dakika ya 17 Liverpool wanapata Kona, Kona Inapigwa na Mohammed Salah lakini wachezaji wa Liverpool wanashindwa Kuitumia Vizuri

Dakika ya 22 Liverpool wanafanya Shambulizi la Nguvu kipa wa Madrid anadaka

Dakika ya 29 Mohammed Salah anashindwa kuendelea na Mchezo baada ya Kuumia, anaingia Lallana

Salah ametoka uwanjani analia akiwa haamini kama anashindwa kuendelea na Mchezo wa Fainali,

Dakika ya 35

Real Madrid 0 – 0 Liverpool

Dakika ya 36 Carvajal naye anashindwa kuendelea na Mchezo baada ya Kuumia naye anatoka analia, Anaingia Nacho

Dakika ya 43 Benzema anaweka Mpira kambani lakini Line 2 anasema tayari ni Offside

HALF TIME

Real Madrid 0 – 0 Liverpool

Dakika ya 51 Benzema anaipatia Bao Real Madrid

Dakika ya 55 Sadio Mane anasaawazisha Goli kwa Liverpool

Real Madrid 1 – 1 Liverpool

Dakika ya 64 Gareth Bale anafunga bao kwa Real Madrid

Dakika 75

Real Madrid 2 – 1 Liverpool

Dakika ya 82 ReaL Madrid wanapata bao la 3 Kupitia kwa Bale anapiga Shuti nje ya 18 mpira Unamshinda Kipa wa Liverpool

Dakika 84

Real Madrid 3- 1 Liverpool (Bale 2,Benzema, Sadio Mane)

FULL TIME

Real Madrid 3- 1 Liverpool (Bale 2,Benzema, Sadio Mane)

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY