Matokeo Yanga vs Mbao Fc 22 Mei 2018

Matokeo Yanga vs Mbao Fc 22 Mei 2018

0

Matokeo Yanga vs Mbao Fc 22 Mei 2018

Matokeo Mechi kati ya Yanga dhidi ya Mbao Fc ni mechi ya 28 kwa Yanga Msimu huu na Mechi ya 29 kwa Mbao Fc msimu Huu. Matokeo ya Mechi Hii ni kama ya Kutafuta heshima Tu kwani Mbao hashuki Daraja na Yanga hawezi kuwa Bingwa.

Tetesi za Usajili Yanga 22 May 2018

Mechi Inaanza saa 10 Kamili na Tutakupa Matokeo Live

tetesi za usajili Simba 22 May 2018

Mechi imeanza katika uwanja wa Taifa

Dakika ya Kwanza Yanga wanaanza kwa shambulizi langoni mwa Mbao Fc

Yanga wanajaribu kupiga Mipira Mirefu katika dakika hizi za Mwanzo

Dakika ya 4 Yusuph Mhilu anakosa nafasi ya Kuipatia Yanga BAO Aliwekewa Mpira mzuri akabaki na Kipa akapiga akakosa, Mpira Ukkarudi tena Kwake anapiga Kipa anadaka

Dakika ya 5 Krosi ya Hassan Kessy inatumiwa Vizuri na Pius Buswita kwa Kichwa lakini inakuwa Chakula kwa Kipa wa Mbao

Dakika ya 6 Mbao wanapata Kona, Inapigwa Kona Fupi Hassan Kessy anawahi na Kutoa Inakuwa Mpira wa Kurushwa Kuelekea Yanga.

Dakika 7

Yanga 0 – 0 Mbao Fc

Dakika 10 Zimeshaondoka uwanja wa Taifa na Matokeo ni 0 kwa 0

Dakika ya 11 Gadiel Michael anapiga Krosi nzuri upande wa Kushoto Kichwa kilichopigwa na Pius Biswita Kinakosa Macho

Dakika ya 17 Raphael Daudi anajaribu Shuti la Mbali mpira unaenda Nje, Ilikuwa nzuri

Dakika ya 19 Maka Edward yupo chini baada ya Kuumia, Anatolewa nje kwaajili ya Matibabu

Dakika ya 20

Yanga 0 – 0 Mbao Fc

Dakika ya 21 Mbao wanapanda na Mpira lakini jalo lililopigwa linapigwa Visivyo

Goaaaaaaal Dakika ya 25 Thaban Kamusoko anapiga Free Kick nzuri na Kuipatia Yanga Bao, Baada ya bao wachezaji wote wanamfata Kocha Mwandila

Yanga 1 – 0 Mbao Fc

Dakika 30

Yanga 1 – 0 Mbao Fc (25′ Thaban Kamusoko)

Toka Mbao wamefungwa bao sasa wanacheza kwa Kufunguka wakijitahidi Kutafuta bao la Kusawazisha

Dakika ya 33 Mbao wanapata Kona lakini Rostand Anaokoa kwa Kupangua.

Dakika ya 35 Pius Buswita leo anaonekana kuwatafuta Waajiri wake wa zamani anapiga Shuti kali nje ya 18 Kipa anapangua.

Dakika ya 43 Thaban Kamusoko anaonekana Kuumia baada ya Kugusana na Mchezaji wa Mbao Fc

Kamusoko anarejea uwanjani na mashabiki wachache waliofika uwanjani wanampigia Makofi

HALF TIME

Yanga 1 – 0 Mbao Fc (25′ Thaban Kamusoko)

KIPINDI CHA PILI

Ametoka Yusuph Mhilu anaingia Matheo Anthony.

Dakika ya 45 Mba wanafanya shambulizi langoni mwa Yanga, Gadiel Anaokoa akiwa kwenye Mwamba wa Goli.

Dakika ya 50 Matheo Anthony aliyeingia Kipindi cha Pili anawachukua Mabeki Npig sHUTI linaenda Nje kidogo ya Lango

Dakika 50

Yanga 1 – 0 Mbao Fc (25′ Thaban Kamusoko)

Dakika ya 52 Matheo anaingia kwa Kasi anapiga shuti mpira Unagonga Mwamba unarudi uwanjani, Matheo anaonyesha uwezo mzuri so Far.

Dakika ya 59 Mbao Fc  wanapata Kona

Dakika 60

Yanga 1 – 0 Mbao Fc (25′ Thaban Kamusoko)

Dakika ya 63 Mbao wanalisakama lango la Yanga

Dakika ya 66 Anatoka Emmanuel Martin anaingia Geofrey Mwashiuya

Dakika 70

Yanga 1 – 0 Mbao Fc (25′ Thaban Kamusoko)

Dakika ya 73 Gadiel Anamimina Mpira Mzuri kwa Buswita anayepiga shuti linalopaa

Dakika ya 75 Maka Edward Anapewa kadi ya Njano wakati huo Paul Godfrey anaingia Kuchukua nafasi ya Raphael Daud

Dakika 75

Yanga 1 – 0 Mbao Fc (25′ Thaban Kamusoko)

Dakika ya 80 Geofrey Mwashiuya anawekewa Mpira Mzuri na Mateo lakini anashindwa kufunga akitazamana yeye na Nyavu

Dakika 85

Yanga 1 – 0 Mbao Fc (25′ Thaban Kamusoko)

MPRIRA UMEKWISHA

Yanga 1 – 0 Mbao Fc (25′ Thaban Kamusoko)

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY