Simba na Azam zamnyemelea mchezaji huyu wa Yanga

Simba na Azam zamnyemelea mchezaji huyu wa Yanga

0

Simba na Azam zamnyemelea mchezaji huyu wa Yanga

Wakati ligi ikiwa inaenda kumalizika leo kwa mechi takribani nane kuchezwa tayari baadhi ya wachezaji wameshaanza mazungumzo na Timu zao na wengine wakiwa wanataka kusajili timu nyingine kutokana tu na Mikataba kuisha.

Moja kati ya wachezaji wa Yanga ambao mikataba yao imeisha ni Nahodha msaidizi Kelvin Yondani “Cotton Juice” .

Yondani mkataba wake umeisha kucheza Yanga na Kuna taarifa za Chini Chini kuwa klabu za Azam na Simba zimeshaanza kufanya naye mazungumzo ya siri kuhakikisha kama Yanga watashindwa kufika dau basi wanamnasa beki huyo Kitasa na ambaye kiwango chake kimekuwa Juu kwa muda mrefu.

Hata hivyo Taarifa nyingine msomaji wa Kwataunit zinaeleza kuwa Yondani ametoa nafasi kubwa zaidi kwa mabosi wake wa sasa Yanga kuweza kuzungumza naye na endapo watakubaliana basi atabaki yanga.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY