Tetesi za Usajili barani Ulaya 29 May 2018

Tetesi za Usajili barani Ulaya 29 May 2018

0

Tetesi za Usajili barani Ulaya 29 May 2018

Manchester City wanakaribia kukamilisha ununuzi wa pauni milioni 75 kwa ajili ya winga raia wa Algeria Riyad Mahrez, mwenye umri wa miaka 27, kutoka Leicester City. (Mail)

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho ana hofu juu ya ushindani wa malipo ya kifedha usajili wa mchezaji wa Wales Gareth Bale kutokana na bei yake, huku Real Madrid ikitarajiwa kumuuza mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 28 kwa bei ya pauni milioni 200 (Express)

Liverpool wako tayari kujiandaa kusaini mkataba na nahodha wa timu ya Lyon Nabil Fekir huku mzungumzo kuhusu uwezekano wa kusaini mkataba wa pauni milioni 60 na mchezaji huyo wa safu ya kati mwenye umri wa miaka 24 yakitarajiwa kuanza wiki hii. (Goal)

 

Mkurugenzi wa soka wa Roma Monchi anasema kuwa hakuna lengo lolote la kumuuza mlinda lango wao Alisson.

Mlinda lango huyo nambari moja mwenye umri wa miaka 25, amekuwa akihusishwa na Liverpool, na taarifa hizo ziliongezeka baada ya kushindwa katika fainali ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya (Mirror)

Manchester United wanamfuatilia kwa karibu mchezaji wa safu ya kati ya Aston Villa Jack Grealish, mwenye umri wa miaka 22, huku wakiangalia namna ya kujijenga siku zijazo. (Sun)

 

Manchester City wamekataliwa kumnunua mchezaji wa kiungo cha kati wa Napoli Jorginho kwa pauni milioni. Klabu hiyo ya Ligi kuu ya Italia (Serie A ) wanataka walipwe pauni milioni 52 kwa mtaliano huyo mwenye umri wa miaka 26, na wanakabiliwa na ushindani kutoka upande wa Chelsea. (Mirror)

Juventus inaweza kumruhusu mshambuliaji Gonzalo Higuain kuondoka kwneye klabu hiyo, ikiwa watapata mkataba unaofaa msimu huu, huku Chelsea wakioongoza katika kutimiza vigezo vya kumchukua raia huyo wa Argentina mwenye umri wa miaka 30. (Calciomercato)

West Ham wako makini kwa mchezaji wa kiungo cha kati wa Fiorentina Milan Badelj. Badelj mwenye umri wa miaka 29 hana mkataba msimu huu, lakini klabu hiyo ya Italia inaamini atasaini mkataba mpya. (Tutto Mercato Web)

 

Mlinzi wa Atletico Madrid Sime Vrsaljko anasema anafurahia kuwa klabu hiyo ya Ligi ya Uhispania, licha ya taarifa kwamba Manchester United wanataka kusaini mkataba na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26, na mchezaji wa kimataifa wa Croatia. (Sportske Novosti – in Croatian)

Newcastle wamepewa fursa ya kusaini mkataba na mlinzi wa zamani wa Liverpool Martin Skrtel, mwenye umri wa miaka 33, kutoka Fenerbahce msimu huu. (Fotomac)

 

Manchester City wako tayari kukamilisha mkataba na Paris St-Germain kwa ajili ya mshambuliaji wa timu ya Monaco mwenye umri wa miaka 19 Kylian Mbappe.

Mfaransa huyo alikuwa katika timu ya PSG kwa mkopo msimu uliopita lakini mabingwa hao wa Ufaransa huenda wakalazimika kuvunja mpango wao wa kumsaini (Manchester Evening News)

 

Samuel Umtiti anayesakwa na Manchester United amefichua taarifa kuhusu utashi wake wa kubakia Barcelona. Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 24 anayecheza safu ya kati – nyuma anasema kuwa hataondoka klabu hiyo ya Uhispania labda afukuzwe. (Sun)

Wakili wa Misri amewasilisha mashtaka ya pauni bilioni moja dhidi ya Sergio Ramos kuhusiana na namna Mohamed Salah alivyoumia katika mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. (Evening Standard)

Meneja wa timu ya Uholanzi Ronald Koeman na kikosi chake wamekuwa wakifurahia masomo ya mchezo wa vishale kutoka kwa raia wa Uholanzi Michael van Gerwen. (Twitter)

Mlinda lango wa Manchester Joe Hart, mwenye umri wa miaka 31, amebadilisha mawakala wake baada ya kutupwa nje ya kikosi kitakachoiwakilisha England katika michuano ya Kombe la Dunia. (Mail)

Credit : BBC

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY