Tetesi za Usajili Yanga 21 May 2018

Tetesi za Usajili Yanga 21 May 2018

1

Tetesi za Usajili Yanga 21 May 2018

Wakati kamati ya Usajili klabu ya Yanga ikiwa imekiri kuwa msimu unaoelekea ukingoni waliyumba kutokana na kutofanya usajili wa Nguvu lakini yote yakiwa ni kutokana na kutokuwa Vizuri kiuchumi.

Hussein Nyika alikiri kuwa hawakuwa vizuri msimu uliopita Ila msimu huu watahakikisha mambo yanakuwa sawa.

WAWILI MTIBWA WATAJWA YANGA

Kuelekea Dirisha Kubwa la Usajili Yanga inatajwa sana kuwarudisha wachezaji wake wawili ambao wamewahi kupita katika klabu ya Yanga ambao kwasasa wapo Mtibwa Sugar.

> magazeti ya Michezo <

Habari ambazo zimeifikia kwataunit.com ni kwamba Kipa wa Mtibwa Sugar Benedict Tinocco ni moja ya Jina ambalo Yanga wanalihitaji katika timu yao kutokana na kuwa kwenye kiwango bora msimu huu.

Tinoco aliwahi kuwa moja kati ya wachezaji wa Yanga japo hakuwahi kuwa na nafasi kwenye kikosi cha Yanga.

Mchezaji mwingine ni Hassan Dilunga ambaye amekuwa mcharo sana msimu Huu akiwa amefunga mabao matano mpaka sasa Ligi kuu huku Azam Sports Federation akiwa amefunga mabao 4.

Dilunga naye ni moja ya wachezaji ambao wanatajwa kuwa wapo kwenye Rada za Yanga kwaajili ya Msimu Ujao wa Ligi.

1 COMMENT

LEAVE A REPLY