USAJILI : Hili la Tshishimbi kwenda Simba bado linachanganya

USAJILI : Hili la Tshishimbi kwenda Simba bado linachanganya

0

USAJILI : Hili la Tshishimbi kwenda Simba bado linachanganya

Leo mida ya Mchana moja kati ya Taarifa zilizokuwa zinatrend kwenye mitandao ya Kijamii zilikuwa ni Taarifa za Simba kumsajili Papy Tshishimbi Kiungo wa Yanga Papy Kabamba Tshishimbi.

Taarifa hizo zikawa zinaakisi maneno ya Haji Manara ambayo alikuwa akiongea na kituo cha EFM kuwa ni lazima waitikise Yanga kama ambavyo Yanga imekuwa ikiwafanyia miaka iliyopita

Manara alikuwa akitumia kauli ya “Kisasi ni Haki” hataki kusema sana ila ni lazima walipe Kisasi kwa watani wao.

UTATA ULIPO.

Kwa Mujibu wa Taarifa zilizoenea wakati Tshishimbi anatua Yanga alisaini mkataba wa Miaka 2 Yanga na baada ya msimu anakuwa amebakiza mwaka Mmoja Yanga.

 

Kwahiyo  msomaji wa Kwataunit kama iko Hivyo basi itakuwa si jambo jepesi Simba kumsajili mchezaji wa Yanga mwenye mkataba wa mwaka Mmoja, Hii haimaanishi kuwa watashindwa hela ya Kumlipa ila Yanga wanaweza wakataka pesa ya Kuikomoa Simba ili ihairishe zoezi Hilo.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY