USAJILI: Ishu ya Simba Kumleta Chris Katongo Hii hapa

USAJILI: Ishu ya Simba Kumleta Chris Katongo Hii hapa

0

USAJILI: Ishu ya Simba Kumleta Chris Katongo Hii hapa

Klabu ya Simba tayari kwa kauli za baadhi ya viongozi na Benchi la Ufundi ni wazi wamepanga kufanya usajili wa Nguvu zaidi msimu ujao kutokana na Kuwa mashindano mengi ya Ndani na yale ya Kimataifa Simba Ikiwa Bingwa wa Tanzania Bara.

Kulingana na Gazeti la Mwanaspoti ambalo limeandika kuwa Limefanya mazungumzo na Lechantre na Kocha kugusia kuhusiana na Usajili wake kama ataendelea kuwa Kocha wa Simba kwaajili ya Msimu Ujao.

Kulingana na Taarifa hiyo Lechantre amelitaja jina la Mshambuliaji Mkongwe Christopher Katongo ambaye anacheza katika timu ya jeshi za Zambia Green Buffaloes.

” Japo huwa sipendi kumweka wazi mchezaji ninayetaka kumsajili mpaka ninapokuwa nimemalizana naye kwa kuogopa umakini wa timu nyingine kuanza kumfatilia lakini miongoni wa ninaowafatilia ni Katongo “

Alisema Lechantre

Katongo ndo yule nahodha aliyeiongoza Zambia Kutwaa ubingwa wa Afrika mbele ya Ivory Coast mwaka 2012.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY