Xclusive: Majibu ya Lipuli kwa Yanga kuhusu kumuomba Adam Salamba

Xclusive: Majibu ya Lipuli kwa Yanga kuhusu kumuomba Adam Salamba

0

Xclusive: Majibu ya Lipuli kwa Yanga kuhusu kumuomba Adam Salamba

Hatimaye Uongozi wa Klabu ya Lipuli kupitia kwa Mwenyekiti wa klabu hiyo Ramadhan Mahano umetoa majibu juu ya nini walichoijibu Yanga kwenye barua yao ya Kumuomba Adam Salamba.

> Habari za Michezo <

Akiongea nasi leo asubuhi Mahano amesema wao kama Lipuli ni kweli wamepokea barua ya Yanga na tayari wameijibu wakiwataka Yanga kutuma Ofa yao.

” Kwanza nataka nikujulishe kwamba Adam Salamba siyo kwamba anatakiwa na timu moja pekee, anatakiwa na Timu mbili na Azam wamewasilisha maombi ya kumhitaji “

alisema Mahano

”  Sisi kama viongozi tumekaa Tumewaambia watuletee ofa mezani tukiona ofa inafaa tutajua wapi anaenda, kama haitufai tutaendelea na mchezo wetu, tunachohitaji kwasasa ni pesa maana hatuwezi kubania riziki ya Mchezaji “

Alimaliza Mahano

Ramadhan Mahano Msomaji wa kwataunit alisisitiza kuwa mambo mengine ataeleza baadae ila kwasasa watu watambue wameijibu Yanga kwa kuwaomba wapeleke Ofa yao.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY