Ametua nchini Kumrithi Meddie Kagere

Ametua nchini Kumrithi Meddie Kagere

0

Ametua nchini Kumrithi Meddie Kagere

Nairobi, Kenya

Mshambuliaji wa Timu ya Kiyovu ya Nchini Rwanda ambaye pia ni raia wa Burundi Francis Mustapha amewasili nchini Kenya katika uwanja wa Jomo Kenyatta International Airport (JKIA) Tayari kwa Usajili.

Mchezaji huyo Francis Mustapha mwenye miaka 22 imeelezwa na C.E.O wa Gor Mahia  Omondi Aduda kuwa mchezaji huyo ni kweli ameshatua Nchini Kenya tayari kwa Usajili.

” Ni kweli Francis Mustapha  ametua Nchini na amekuja na meneja wake, Tutakaa nao mezani ili kuweza kukamilisha Usajili wake, Nafikiri ndiye atakayemrithi Meddie Kagere sababu hilo ndilo tunalorifikiria kwa sasa “

Naye mchezaji Francis Mustapha akizungumza na Kwataunit.co.ke nchini Kenya  amesema kuwa Gor Mahia ni timu ambayo alikuwa anawaza kuichezea siku moja na toka alipoiona ikicheza na Rayon Sports kombe la Shirikisho barani Afrika aliona kabisa ni Timu inayomfaa kucheza.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY