Anasubiriwa Kocha tu mchezaji huyu atue Yanga

Anasubiriwa Kocha tu mchezaji huyu atue Yanga

0

Anasubiriwa Kocha tu mchezaji huyu atue Yanga

Ukizungumza timu ambazo huwa zinatoa wachezaji wenye vipaji basi bila shaka Mtibwa Sugar ni moja kati ya Vilabu hivyo na sasa Upepo wa Yanga umeelekea Mtibwa kwa Mara nyingine.

Upepo wa Yanga baada ya uwepo wa tetesi za Kumnasa Bennedict Tinocco ambaye ni Kipa wa Mtibwa unaambiwa mchezaji mwingine wa Mtibwa yupo kwenye mikono salama ya  mwenyekiti wa kamati ya usajili Yanga Hussein Nyika.

Taarifa za Kuaminika ambazo kwataunit imezipata zinadai kuwa Nyika ameshafanya mazungumzo na Mchezaji Salum Kihimbwa wa Mtibwa Sugar na Kama kocha Mwinyi Zahera ambaye ameshatua Nchini atakubali uwezo wake basi atasaini Yanga kwaajili ya Msimu Ujao.

Image result for salum kihimbwa

Inaelezwa Salum Kihimbwa ambaye ameonyesha uwezo mkubwa sana msimu wa Ligi kuu na hata kombe la Azam Sports Federation ameshaanza kuwaaga hata baadhi ya watu wake wa Karibu kuwa msimu ujao huenda asiwepo Manungu na Mtibwa Sugar.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY