Deal Done: KMC Yamsajili Mbabe Wa Simba

Deal Done: KMC Yamsajili Mbabe Wa Simba

0

Kwa habari za Papo kwa papo Simba,yanga na Nyingine Like Ukurasa wetu wa facebook HAPA

Klabu ya KMC FC imetangaza kumsajili mlinda mlango wa zamani wa klabu za Simba na Yanga, Juma Kaseja kuitumikia klabu hiyo kwa msimu wa mwaka 2018/2019.

Kaseja amejiunga na klabu hiyo akitokea kwa “Wanankurukumbi ” Kagera Sugar ambapo ametumika kwa msimu wa 2017/2018 kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Juma Kaseja golikipa mwenye uzoefu zaidi na aliyepata kupita katika klabu mbalimbali hapa Tanzania na kufanya vizuri katika mashindano ya kimataifa pia akiitumikia Taifa stars kwa vipindi tofauti amejiunga rasmi na klabu ya @kmcfc_official _official yenye maskani yake Kinondoni Dar es salaam kwa mkataba wa mwaka mmoja. Hii ni moja ya sajili na majina makubwa ambayo yanatarajia kutua katika klabu hii iliyopanda daraja na kushiriki ligi kuu ya Tanzania bara msimu wa 2018/19.

Ikumbukwe Kaseja aliiongoza Kagera Sugar kuharibu rekodi ya Mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara baada ya kutoa mkwaju wa Penati ambao ungewapatia simba bao na kuifanya Kagera Sugar kuibuka kidedea kwa ushindi wa goli 1-0.

Punguza matumizi ya MB downoload App Bora ya Michezo BONYEZA HAPA

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY