Habari Mpya Kutoka Simba Asubuhi Hii, Ni Kuhusu Usajili wa Beki Kutoka...

Habari Mpya Kutoka Simba Asubuhi Hii, Ni Kuhusu Usajili wa Beki Kutoka Ivory Coast

0

Habari Mpya Kutoka Simba Asubuhi Hii, Ni Kuhusu Usajili wa Beki Kutoka Ivory Coast

Beki wa zamani wa klabu ya Azam Fc raia wa Ivory Coast Pascal Wawa yupo jijini Dar kwa ajili ya mazungumzo ya mwisho ili kujiunga na klabu ya Simba Sc.

Wawa ambaye ni mchezaji huru ametua Dar jana na kupokelewa na mratibu wa klabu ya Simba, Ally Abbas na kupelekwa moja kwa moja kwa viongozi wakubwa wa klabu ya Simba na jana wakafanya mazungumzo ya mwisho kuhusu kuitumikia klabu hiyo na jioni akaungana na kikosi cha Simba kwenye mazoezi.

-Habari za uhakika kutoka ndani ya klabu hiyo Pascal Wawa ataanza mazoezi rasmi leo kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya Kagame Cup itakayoanza siku ya Ijumaa June 29 huku Simba wakianza Jumamosi ya June 30 na Dakadaha ya Somalia katika uwanja wa Taifa Dar.

-Klabu ya Simba imempa ofa ya mkataba wa mwaka mmoja Paschal Wawa kuitumikia klabu hiyo ila atasaini mkataba baada ya kuisha kwa michuano ya Kagame Cup hivyo Simba wanataka kumuona kwanza kwenye kombe la Kagame Cup huku wakala wake akiwagomea Simba mteja wake (wawa) kufanyiwa majaribio.

-Alipotafutwa Mratibu wa Simba, Ally Abbasi alisema
“Kazi yangu si kujua nani amesajiliwa kwa mkataba wa miaka mingapi mimi nimefanya kazi yangu nimemaliza kuhusu kama Wawa wamemalizana na viongozi atafutwa Kaimu Rais”

-Iwapo Simba watakamilisha usajili wa Paschal Wawa atakuwa mchezaji wa nne Mpya kusajiliwa msimu huu kwani tayari walishasajili washambuliaji wapya watatu Marcel Kaheza kutoka Majimaji, Adam Salamba kutoka Lipuli na Mohamed Rashid kutoka Tz Prisons.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY