Haji Manara Baada Ya Simba Kumtambulisha Kagere Na Wenzake

Haji Manara Baada Ya Simba Kumtambulisha Kagere Na Wenzake

0

Haji Manara Baada Ya Simba Kumtambulisha Kagere Na Wenzake

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Simbasc Haji Manara, amesema klabu hiyo bado itaendelea kusajili licha ya kuwatambulisha Meddie Kagere, Paschal Wawa na Deogratius Munish Dida mbele ya Waandishi wa Habari hiyo jana.

“Hatufanyi hivi kwa ajili ya kumfurahisha mtu bali ni mipango ya dhati kuhakikisha Simba inakuwa na kikosi kipana kinachoweza kufanya vizuri”. Alisema Haji Manara

Wawakilishi hao wa Tanzania kwenye ligi ya Mabingwa Afrika, mbali na mashindano hayo watakabiliwa na mashindano mengine mengi ikiwemo Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara, Kombe la Mapinduzi, Azam Sports Federation CUP, SportPesa Super CUP na KAGAME hivyo ni lazima wawe na kikosi kipana na cha ushindani.

Mbali na hilo timu hiyo ina deni kubwa toka kwa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John P Magufuli ambaye aliagiza klabu hiyo iwe ya kwanza kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika au walau iweze kufika fainali ya mashindano hayo.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY