Haya ndiyo matokeo ya GorMahia baada ya Kucheza bila Kagere

Haya ndiyo matokeo ya GorMahia baada ya Kucheza bila Kagere

0

Haya ndiyo matokeo ya GorMahia baada ya Kucheza bila Kagere

Timu ya Gor Mahia leo ilishuka uwanjani kucheza mchezo wake wa Ligi Kuu ya kenya maarufu zaidi kama Sportpesa Premier League.

Gor Mahia ikicheza bila Mshambuliaji wake wa Kutumainiwa Meddie Kagere ambaye yupo Tanzania kwasasa leo akiwa amesaini kandarasi ya Miaka miwili kuchezea ndani ya Klabu ya Simba.

Katika mchezo wa leo Gor Mahia wamefanikiwa kupata ushindi wa bao 5 kwa 0 wakicheza na Posta Rangers, Magoli ya mabingwa hao wa Kenya na Sportpesa Super Cup yamefungwa na Tuyisenge, Guikan, George Odhiambo “Blackberry ” aliyeingia nyavuni mara mbili na bao la tano likifungwa na Lawrence Juma.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY