Hii ni habari njema kwa Yanga leo 19 June 2018

Hii ni habari njema kwa Yanga leo 19 June 2018

0

Hii ni habari njema kwa Yanga leo 19 June 2018

Katika kipindi ambacho Yanga walikuwa wanakosa raha ni pale walipokuwa wakisikia mchezaji wao anahitajika kwenye timu fulani kwaajili ya Usajili.

Hali hiyo ilikuwa inatokana na Hali ya Kiuchumi ndani ya Klabu ya Yanga hivyo kama timu zenye mkwanja kama Azam Fc na Simba zingewahitaji wachezaji waliomaliza mkataba Yanga ingekuwa ni kazi nyepesi Tu.

Mmoja ya wachezaji ambao Walianza kutajwa sana kutoka Yanga kwenda Azam Fc  msomaji wa Kwataunit.co.ke alikuwa ni Juma Abdul Mnyamani, Lakini habari nzuri kwa wana Yanga ni kwamba Azam Fc wameamua Kuachana na dili Hilo.

Azam inaelezwa kuwa wameamua kuachana na dili hilo kutokana na kumnasa beki Mganda Nicolas Wadada kutoka Vipers ya Nchini Uganda kwahiyo itakuwa Rahisi kiasi kwa Yanga kumbakiza Juma Abdul kwaajili ya Msimu Ujao.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY