Huu Ndio Ujumbe Mzito Aliouacha Mbenini Wa Yanga Wakati Anaondoka

Huu Ndio Ujumbe Mzito Aliouacha Mbenini Wa Yanga Wakati Anaondoka

0

Huu Ndio Ujumbe Mzito Aliouacha Mbenini Wa Yanga Wakati Anaondoka

Mchezaji ambaye alikuwa akitazamiwa kuziba pengo la Obrey Chirwa Yanga, Mbenini Marcellin Koukpo ameripotiwa kuondoka klabuni hapo huku akiacha ujumbe mzitokuhusiana na soka la Tanzania.

Instagram mchezaji huyo ameposti picha akiwa katika ndege ndege akisema kuwa mpira wa Tanzania hautoweza kuendelea kutokana na watu wa kati.

Kwa kutumia lugha ya Kiingereza, mshambuliaji huyo raia wa Benin alisema, “Bye Bye,” ikiwa ni kama anaaga.

Baada ya watu kutoa maonı yao akajıbu kuwa, “Tanzania football will drom due to the middlemen in the football industry,” akiwa anamaanishwa kwamba, soka la Tanzania siku zote litaendelea kwenda chini sababu ya madalali walioko katika mpira.

Kwa kauli hii inaonesha dhahiri kwamba mchezaji huyo amechemka Yanga na anarejea kwao.

Koukpo alikuja kufanya majaribio kwa ajili ya kujiunga na Yanga na ni wiki sasa alikuwa jijini Dar es Salaam alikokuwa anasubiriwa na kocha mkuu wa timu hiyo Mwinyi Zahera.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY