Huyu Hapa Mrithi Wa Kagere Gormahia Baada Ya Kutua Simba

Huyu Hapa Mrithi Wa Kagere Gormahia Baada Ya Kutua Simba

0
Huyu Hapa Mrithi Wa Kagere Gormahia Baada Ya Kutua Simba.

Mara baada ya mshambuliaji wa klabu ya Gor Mahia, Meddie Kagere kujiunga na wekundu wa msimbazi tayari timu hiyo imeweka bayana kuwa mrithi wa nyota huyo huenda akawa mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Uganda, Erissa Ssekisambu.

Ssekisambu aliwasili juzi nchini Kenya kwa ajili ya kukamilisha uhamisho wake wa kujiunga na mabingwa hao wa Kenya.

Aidha Mchezaji huyo amenukuliwa na vyombo vya habari nchini Uganda akisema hana mpango wa kusalia na mabingwa wa soka nchini Uganda, Vipers ambao amewatumikia kwa takribani miaka mitatu.

Ikumbukwe kuwa Ssekisambu anajiunga na Gormahia ili kuziba pengo lililoachwa na mkali wa Mabao, Kagere licha ya kua mipango ya Kocha Kerry ilikuwa ni kuwatumia nyota hawa kwa pamoja.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY