Jibu alilolitoa Lechantre alipoulizwa kwanini hajakaa Benchi

Jibu alilolitoa Lechantre alipoulizwa kwanini hajakaa Benchi

0

Jibu alilolitoa Lechantre alipoulizwa kwanini hajakaa Benchi

Jana story Kubwa iliyokuwa imetanda kwa watu wengi ilikuwa ni suala la Kocha mkuu aliyeipa Ubingwa Sinba baada ya Muda Mrefu Pierre Lechantre kuonekana amekaa benchi wakati kila mtu anaelewa kuwa yeye ndiye Kocha Mkuu.

Kila mtu aliongea lake na Kila mtu aliandika Lake lakini katika mchezo wa jana moja kati ya watu walionekana kuwa karibu na Kufanya naye mazungumzo alikuwa ni Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Mwanaspoti Gift Macha.

Gift Macha wa Mwanaspoti alionekana akiongea na Pierre Lechantre wakati mechi ikiendelea na Kulingana na maelezo yake Pierre alifunguka haya.

” Nimempa nafasi Djuma aonyeshe uwezo wake kwani mkataba wangu umeshamalizika  na nasubiri kufahamu hatma ya Mkataba wangu mpya “

Inadaiwa Mkataba wa Lechantre umeisha toka May 29 na Inadaiwa viongozi wa Simba wamekuwa wakimpiga danadana Lechantre kumuongezea Mkataba.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY