Kati ya Simba na Yanga unaambiwa Pascal Wawa anatua Huku

Kati ya Simba na Yanga unaambiwa Pascal Wawa anatua Huku

0

Kati ya Simba na Yanga unaambiwa Pascal Wawa anatua Huku

Timu mbalimbali zinakomaa kweli kweli kuhakikisha zinasajili wachezaji wa maana na wanaoweza kuja kusaidia timu zao kwaajili ya msimu ujao wa Mashindano mbalimbali.

Moja ya Timu hizo ni WAPINZANI wa jadi nchini yani Simba na Yanga na sasa limeibuka suala la timu zote kutajwa kwa Mlinzi wa zamani wa Azam Fc Pascal Wawa.

Kulingana na Chanzo chetu cha Uhakika Simba ndiyo waliokuwa wa Kwanza kufanya mazungumzo na Wawa mwezi April lakini baada ya mazungumzo taarifa zinadai hawakurudi tena.

Yanga nao wakafanya mazungumzo na Wawa ambaye aliondoka Azam na Kujiunga na El Merreikh ya Sudan na wakakubaliana baadhi ya mambo na Kilichobaki kilikuwa ni pesa ya Usajili Tu.

Na alipotafutwa Wawa Mwenyewe alikiri kufanya mazungumzo na Timu hizo lakini akasema Yanga wameonekana kumwitaji Zaidi kuliko Simba, Kwahiyo msomaji wa kwataunit kama mambo yatakaa sawa Huenda Pascal Wawa akavaa uzi wa Yanga msimu ujao.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY