Kikosi cha Simba kinachoweza kuanza dhidi ya Gor mahia leo

Kikosi cha Simba kinachoweza kuanza dhidi ya Gor mahia leo

0

Kikosi cha Simba kinachoweza kuanza dhidi ya Gor mahia leo

Hiki ni Kikosi cha Utabiri cha Simba kinachoweza Kuanza kwenye Mchezo wa Fainali ya Sportpesa kati ya Simba Na Gor Mahia

Golini : Bila Shaka ataanza Aishi Manula ambaye amekuwa msaada Mkubwa na Kuisaidia Timu kufika hatua ya Fainali.

Mabeki wa pembeni : Namba Mbili Shomari Kapombe na Upande wa Kushoto Le Captaaain Mohammed Hussein ” Zimbwe Jr”

Mabeki wa Kati : Kuna mabeki watatu msomaji wa Kwataunit  lakini wawili ndiyo wanatakiwa Kuanza Yusuph Mlipili, Paul Bukaba na Erasto Nyoni kwa aina ya Mchezo wa Leo naona nafasi ya Yusuph Mlipili na Erasto Nyoni wakianza pamoja.

Viungo wa Kati : Namba 6 Jonas Mkude na Namba 8 anaweza kuanza Mzamiru Yassin.

Mawinga : Namba 7 Shiza Kichuya na namba 11 Rashid Juma ambaye ni kinda ambaye amekuwa na kiwango bora mechi 2 zilizopita.

Mastraika : Tisa na 10 LEO bila shaka watasimama Mohammed Rashid na Adam Salamba.

KIKOSI HALISI TUTAKUWEKEA BAADAYE BAADA YA KUTOKA

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY