Kocha anayetajwa kutua Simba baada ya Lechantre kuondoka

Kocha anayetajwa kutua Simba baada ya Lechantre kuondoka

0

Kocha anayetajwa kutua Simba baada ya Lechantre kuondoka

Siku kadhaa mara baada ya kocha Mkuu wa Simba kuamua kufunga Vioo kwa Simba kwanza akionekana kugoma Kukaa benchi wakati wa mechi ya Nusu Fainali Sportpesa kati ya Simba Na Kakamega.

Kisha Kocha huyo kuondoka Kenya na Kurejea Tanzania ikielezwa kuwa alifata maslahi yake na Kufanya mazungumzo na Viongozi wa Juu ili wamalizane na Aondoke.

Sasa kuna tetesi kuwa Simba wamepanga kumfanya Kocha Masoud Djuma kipenzi cha washabiki wengi wa Simba kuwa Kocha Mkuu wa Simba huku msaidizi wake mipango inawekwa mikoba ichukuliwe na Kocha Suleiman Matola.

Matola kwasasa ni kocha wa Timu ya Lipuli Fc ya Mkoani Iringa na amewahi kucheza na Kufundisha Simba kwa Nyakati tofauti kama kocha MSAIDIZI.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY