Majibu kutoka Simba kama Bocco na Okwi wataungana na Timu Kenya haya...

Majibu kutoka Simba kama Bocco na Okwi wataungana na Timu Kenya haya hapa

0

Majibu kutoka Simba kama Bocco na Okwi wataungana na Timu Kenya haya hapa

Mara baada ya Mchezo kati ya Kariobangi Fc na Simba kumalizika na Simba kushinda kwa taabu kwa njia ya Matuta mara baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare ya bila Kufungana washabiki na wapenzi wengi wa Simba wameanza kuhoji kuhusu Bocco na Okwi.

Okwi na Bocco hawakuungana na Simba na Baadhi ya Taarifa zilidai kuwa huenda wangeungana na Timu baadaye ikiwa nchini Kenya lakini majibu ya Haji Manara kama wachezaji hao wataungana na Timu yametolewa jioni ya Leo kuwa hawataweza Kuungana na Timu.

” Bocco anaumwa alimaliza ligi akiwa anaumwa, Okwi ameumia akiwa Timu ya taifa ya Uganda kwahiyo hatutaongeza mchezaji mwingine labda Salamba kesho anaweza Kuungana na Timu “

 

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY