Matokeo AFC Leopards vs Singida United 5 June 2018

Matokeo AFC Leopards vs Singida United 5 June 2018

0

Matokeo AFC Leopards vs Singida United 5 June 2018

Matokeo ya Mechi kati ya AFC Leopards ya Kenya dhidi ya Singida United kutoka Tanzania, Mechi ikichezwa katika uwanja wa Afraha mjini Nakuru Kenya.

Kuanzia saa tisa tutakuletea Mechi Live

Mechi Imeanza katika uwanja wa Afraha Nakuru

Leopards 0 – 0 Singida United

Dakika ya 2 Tu Singida Wanapata Kona, Inapigwa Kipa anatoa na kuwa Mpira wa Kutupa

Dakika ya 6 Lubinda Mundia anajaribu kujitwisha Mpira kwa Kichwa lakini Kipa anauona na Kudaka

Singida United wanaonekana kuanza Vizuri zaidi kuliko AFC Leopards kwa dakika 8 za Mwanzo, Matokeo bado ni 0 kwa 0

Dakika 10

AFC Leopards 0 – 0 Singida United

Singida wanaendelea kucheza vizuri wakiwashika kisawasawa Chui eneo la kati ya Uwanja

Dakika ya 20

AFC Leopards 0 – 0 Singida United

Dakika ya 22 AFC Leopards wanafanya shambulizi zuri , Manyika Jr anatoa na Kuwa Kona

Dakika ya 24 Leopards wanafanya tena Shambulizi la Maana Langoni mwa Singida Manyika Jr Anakuwa Shujaa kwa mara Nyingine anaudaka Mpira

DDakika ya 27 Danny Lyanga anashindwa Kuifungia Singida Bao, Mpira Ulipigwa na Kenny Ally kipa wa Leopards Owande akashindwa Kuudaka ukarudi uwanjani Lyanga ankajaribu Kuuweka sawa lakini mpira Ulikuwa kasi sana na Ukatoka

Dakika 30

AFC Leopards 0 – 0 Singida United

Dakika ya 35 Bado ni 0 kwa 0 kATIKA uwanja wa Afraha

Dakika ya 41 AFC Leopards wanapata Kona baada ya Manyika Kupangua Shuti lililopigwa Golini na Mabeki kuokoa

HALF TIME

AFC Leopards 0 – 0 Singida United

KIPINDI CHA PILI

Dakika ya 60

AFC Leopards 0 – 0 Singida United

Dakika ya 69 AFC Leopards wanapata Penati baada ya MCHEZAJI wa Leopards Kuangushwa

Dakika ya 70 AFC wanakosa Penati hapa, Manyika anaokoa kwa Kupangua, Inapigwa Tena anaokoa kwa Mguu na Kisha anaudaka

Dakika 10 zimesalia katika uwanja wa Afraha Nakuru matokeo yakiwa bado ni Tasa

Dakika ya 85

AFC Leopards 0 – 0 Singida united,  Leopards wamekuja Juu zaidi kwasasa wakitengeneza nafasi nyingi kuliko Singida United

DAKIKA 90 ZIMEISHA

AFC Leopards 0 – 0 Singida United

ZINAFUATA PENATI

Kenny Ally anakosa penati ya Kwanza ya Singida United

Leopards wanapata penati yao ya Kwanza

AFC Leopards 1 – 0 Singida United

Shafiq Batambuze anafunga penati ya Pili ya Singida United

Leopards wanakosa penati ya Pili

AFC Leopards 1 – 1 Singida United

Miraji Adam anafunga penati ya 3 kwa Singida United

AFC leopards wanakosa penati yao ya Tatu, Inapigwa Nje kabisa ya Uwanja

AFC Leopards 1 – 2 Singida United

Danny Lyanga anafunga penati ya NNE kwa Singida United

AFC Leopards wanapata penati yao ya NNE

AFC Leopards 2 – 3 sINGIDA United

Ellynyesia Sumbi anafunga penati ya 5 kwa Singida United

AFC Leopards 2 – 4 Singida United

Singida United wanafuzu hatua ya Nusu Fainali

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY