Matokeo Kombe La Dunia Belgium vs Tunisia.

Matokeo Kombe La Dunia Belgium vs Tunisia.

0

Matokeo Kombe La Dunia Belgium vs Tunisia.

Timu ya taifa ya Ubelgiji imeinyuka timu ya taifa ya Tunisia jumla ya magoli 5-2 katika mchezo wa pili wa kundi G na kujihakikishia nafasi ya kusonga mbele katika hatua ya 16 bora ya michuano hiyo.

Belgium imewachukua dakika 6 kuanza kuandika karamu ya magoli kupitia kwa Eden Hazard kwa mkwaju wa penati kabla Bronn kuisawazishia Tunisia.

Magoli ya Lomelu Lukaku mawili yakaifanya Belgium dakika ya 16 na 45 kabla ya Hazard kuongeza goli la tatu mnamo dakika ya 51.

Batshuayi na Khazri ndio walio tamatisha karamu ya magoli huku Batshuayi akifunga goli la tano kwa Belgium na Khazri kuifungia Tunisia goli la pili.

Hadi dakika 90 zinakamilika Belgium 5 Tunisia 2. Kwa matokeo hayo Tunisia imejiwekea mazingira magumu ya kusonga mbele kutokana na kupoteza mechi zote mbili ambazo imeshacheza.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY