Matokeo Simba vs Kakamega Homeboyz leo 7 June 2018 Sportpesa

Matokeo Simba vs Kakamega Homeboyz leo 7 June 2018 Sportpesa

0

Matokeo Simba vs Kakamega Homeboyz leo 7 June 2018 Sportpesa

Matokeo ya Moja kwa Moja na Kwataunit mechi kati ya Simba dhidi ya Kakamega Homeboyz (Simba vs Kakamega Homeboys 7 June 2018)

Mechi Imeanza Afraha Stadium

Kakamega 0 – 0 Simba

Dakika ya 2 wakati Kakamega Homeboyz wanajaribu kushambulia line 2 anaonyesha ni Offside

Dakika ya 6 Simba leo imeanza kwa Mchezo wa Kasi ukilinganisha na Mchezo uliopita ambao walikuwa wamepooza

Dakika ya 7 Mpira Unapigwa Krosi na Shomari Kapombe beki wa KK Homeboys anatoa na Kuwa Kona.

Inapigwa Kona fupi mchezaji wa Simba anakosa Mpira na Inakuwa Hatari langoni mwa Simba baada ya Mchezaji wa Kakamega Kukimbia na Mpira lakini manula anauwahi na Kuudaka

Dakika ya 10

Kakamega Homeboyz 0 – 0 Simba

Dakika ya 11 Simba wanapata Kona ya Pili, Inapigwa KIPA ANADAKA

Dakika ya 12 Rashid Juma anashindwa kutumia nafasi anayoipata anapiga mpira mabeki wanazuia

Dakika 15

KK Homeboys 0 – 0 Simba

Dakika ya 22 Allan Wanga anajaribu kufanya yake langoni mwa Simba lakini Kontroo yake inakuwa Mbovu

Dakika 25

Kakamega Homeboyz 0 – 0 Simba

Dakika ya 27 Offside Allan Wanga

Dakika ya 28 Wafula anajaribu shuti kali lakini linapaa juu ya Lango la Simba.

Dakika ya 28 Kakamega nao wanapata Kona

Dakika 30

Matokeo Kakamega Homeboys vs Simba

KK Homboys 0 – 0 Simba

Dakika ya 34 Kakamega wanafanya Shambulizi Zuri langoni mwa Simba, Mpira unapalaza nyavu za Juu

Dakika ya 35 Shiza Kichuya anajaribu shuti langoni mwa Kakamega mpira Unapita pembeni ya Goli

Dakika ya 37 Haruna Niyonzima anapiga Shuti la Kukata kipa anatoa na Kuwa kona

Dakika ya 42 Mohammed Rashid anajaribu kupiga Shuti langoni lakini kipa anauona Mpira anadaka, Bado 0 – 0

HALF TIME

Kakamega Homeboyz 0 – 0 Simba

KIPINDI CHA PILI

Kipindi cha pili

Dakika ya 46 Mohammed Rashid anawekwa chini karibu na Kibendera, Faulo

Dakika ya 50

KK Homeboyz 0 – 0 Simba

Dakika ya 56 Simba wanapata Kona , Inapigwa kona Inakosa Madhara.

Dakika ya 58 Simba wanakoswa Goli.

Dakika ya 58 Jonas Mkude anapewa kadi ya Njano

Dakika ya 58 Adam Salamba mwenye jezi namba 11 Anaingia nafasi ya Rashid Juma ambaye ameshindwa kuendelea baada ya Kuumia

Dakika ya 65

KK Homeboyz 0 – 0 Simba

Dakika ya 69 Anatoka Mohammed Rashid anaingia Moses Kitandu

Dakika ya 74 Kitandu anapata nafasi ya wazi anapiga Kipa anadaka

Dakika ya 80 Kichuya anapiga Faulo nzuri lakini inakosa Mtu wa kumalizia

Kakamega Homeboyz 0 – 0 Simba

Dakika ya 85

KK Homeboyz 0 – 0 Simba

Dakika ya 89 Allan Wanga anapiga Kichwa , Manula anasafiri na Kuudaka Mpira, Ulikuwa uzame langoni

FULL TIME

Kakamega Homeboys 0 – 0 Simba

ZINAFUATA PENATI

Allan WA Homeboys anafunga penati ya Kwanza

Haruna Niyonzima anafunga penati Upande wa Simba

KK Homeboys 1 – 1 Simba

Homeboys wanapata penati yao ya Pili

Erasto Nyoni anafunga penati upande wa Simba

KK Homeboys 2 – 2 Simba

Wafula wa Homeboys anafunga penati ya 3 ya Homeboys

Shomari Kapombe anafunga penati kwa Simba

KK Homeboys 3 – 3 Simba

Esiye anafunga upande wa KakamegaHomeboys

Shiza Kichuya anafunga upande wa Simba

KK Homeboys 4 – 4 Simba

Opondo wa Kakamega anakosa Penati ya Mwisho

Jonas Mkude anafunga penati

KK Homeboys 4 – 5 Simba, Simba wanaingia Fainali ya Sportpesa Super Cup

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY