Matokeo Simba vs Kariobangi Sharks leo 4 June 2018

Matokeo Simba vs Kariobangi Sharks leo 4 June 2018

0

Matokeo Simba vs Kariobangi Sharks leo 4 June 2018

Haya ni Matokeo ya Moja kwa Moja kati ya Simba dhidi ya Kariobangi Sharks ya Kenya michuano ya Sportpesa Super Cup iliyoanza Jana.

Timu zinaingia uwanjani kwasasa

Mechi Imeanza katika uwanja wa Afraha

Kariobangi Sharks 0 – 0 Simba

Dakika ya 2 Simba wameanza kwa Kupiga Pasi fupi fupi wakitengeneza Mashambulizi

Dakika ya 3 K Sharks wanapata Kona ya Kwanza, Inapigwa mabeki wanaokoa inarudishiwa na K Sharks lakini mpira Unapaa nje ya Lango

Dakika 5

K Sharks 0 – 0 Simba

Dakika ya 6 K Sharks wanajaribu kutengeneza Shambulizi Manula anatoka Nje ya Eneo lake na Kuokoa kwa Kichwa

Dakika 10

K Sharks 0 – 0 Simba

Dakika ya 14 Mchezaji wa Kariobangi SHARKS anakosa goli akiwa amebaki yeye na Aishi Manula

Dakika 20

K Sharks 0 – 0 Simba

Dakika ya 25 K Sharks wanapata Kona, wanashindwa Kuitumia

Dakika ya 31 Mo Ibrahim Anajaribu shuti nje ya 18 kipa Anadaka

Dakika ya 40 Rashid Juma anaingia kuchukua nafasi ya Ally Shomari

Dakika ya 44 Haruna Niyonzima anajaribu shuti la mbali lakini linakuwa chakula kwa Kipa wa Kariobangi

HALF TIME

Kariobangi Sharks 0 – 0 Simba

KIPINDI CHA PILI

Marcel Kaheza ameingia kipindi cha Pili kuchukua nafasi ya Mo Ibrahim

Dakika ya 55

Simba wameanza kucheza kwa kasi tofauti na Kipindi cha Kwanza

K Sharks 0 – 0 Simba

Dakika ya 59 Haruna Niyonzima anapewa kadi ya njano kwa Kupinga maamuzi ya Refarii

Dakika ya 64 Sharks wanapata kona ya 3 ya Mchezo.

Dakika ya 65 Marcel Kaheza aliyeingia kipindi cha Pili anatoka anaingia Shiza Ramadhan Kichuya

Dakika ya 70

Kariobangi Sharks 0 -0 Simba

Dakika ya 74 Kariobangi wanafanya shambulizi zuri wakati Bukaba Akijitahidi kuokoa anagongana na Manula wote wapo chini

Dakika ya 80

Sharks 0 – 0 Simba

Mpira Unaendelea Manula anaendelea lakini bado anachechemea, Amefungwa Bandage eneo la Goti alipogongana na Mlinzi wake Bukaba

Dakika ya 83 Anatoka Mohammed Rashid anaingia Moses Kitandu upande wa Simba

Dakika 6 za Nyongeza Afraha Stadium

Sharks 0 – 0 Simba

Mzamiru yassin anaingia dakika za Nyongeza

DAKIKA 90 ZIMEMALIZIKA

Sharks 0 – 0 Simba

ZINAFUATA PENATI

Sharks wanakosa penati ya kwanza

Niyonzima anapata Penati upande wa Simba.

Sharks 0 – 1 Simba

Aishi Manula anadaka penati ya pili ya Sharks

Mohammed Hussein Anakosa Penati ya Pili ya Simba

Kiprikui anafunga penati kwa Sharks

Erasto Nyoni anafunga penati kwa Simba

Sharks 1 – 2 Simba

K Sharks wanapata Penati yao ya nne wakiwa Wamefunga Mbili

Paul Bukaba anakosa penati upande wa Simba

Sharks 2 – 2 Simba (Baada ya kila timu kupiga penati 4)

Aishi Manula kwa mara Nyingine anacheza penati za Sharks

Goaaaaaal Jonas Mkude anapata penati ya 5

Sharks 2 – 3 Simba

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY