Meddie Kagere kutua Yanga huenda Ikawa rahisi kutokana na Hili

Meddie Kagere kutua Yanga huenda Ikawa rahisi kutokana na Hili

0

Meddie Kagere kutua Yanga huenda Ikawa rahisi kutokana na Hili

Yanga inatajwa kuwa katika mazungumzo na wachezaji takribani wanne wa Gor Mahia ya Kenya, Moja ya wachezaji ambao wamekuwa wakitajwa zaidi katika hao wanne ni Mrwanda ambaye alizaliwa Uganda Meddie Kagere.

Kagere msomaji wa Kwataunit anatajwa zaidi Yanga kutokana na safu ya Ushambuliaji klabu ya Yanga kuonekana kupungua makali yake kwa msimu wa Ligi uliomalizika.

URAHISI WA KAGERE KUTUA YANGA.

Kama ulifikiri inaweza ikawa shughuli sana kwa Straika Huyo mwenye kasi, Nguvu na Uwezo wa Kufunga magoli katika mazingira yote basi utakuwa Unajidanganya.

Ukweli ni Kwamba Kagere amemaliza Mkataba wake na Gor Mahia hivyo ni mchezaji huru na Timu yoyote itakayoweza kufika dau basi inaweza Ikamnasa Nyota huyo anayeongoza Kwa Magoli Sportpesa Super Cup mpaka sasa kabla ya Fainali.

Mchezaji ambaye anakuwa na Mkataba na Timu yake huwa ni ngumu kidogo kumsajili kwani itabidi uvunje Mkataba na Timu yake kwa Kulipa hela ya Kuvunja Mkataba na Kisha kuzungumza na Mchezaji naye umlipe pesa ya Usajili.

Lakini Yanga kazi huenda Ikawa Nyepesi kwa Meddie Kagere kwani itawalazimu kuzungumza na mchezaji pekee kisha mambo yanakuwa Yameiva.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY