Rage achekelea Yanga kupokwa wachezaji na Simba atamani na hawa waondoke

Rage achekelea Yanga kupokwa wachezaji na Simba atamani na hawa waondoke

0

Rage achekelea Yanga kupokwa wachezaji na Simba atamani na hawa waondoke

Mwenyekiti wa zamani wa Klabu ya Simba Ismail Aden Rage amefunguka na Kusema kuwa anafurahia sana kuona Simba wanasajili wachezaji ambao Yanga walikuwa kwenye mipango ya Kuwasijili.

Akizungumza leo kupitia kipindi cha Michezo cha EFM Rage amefunguka Yanga waliwahi kuwazunguka na Kumsajili Mbuyu Twitte licha ya kuwa tayari walikuwa wameshamalizana naye kwa Kumlipa dola elfu 40 za Kimarekani.

Rage amefunguka Pia anatamani Simba waweze kuwashawishi wachezaji wa Yanga kama Kelvin Yondani na Papy Kabamba Tshishimbi waweze kwenda timu nyingine.

Ili Yanga ikose kabisa Nguvu kwani akikumbuka walichowahi kumfanyia kwa Twitte hawezi kusahau kwani Yanga walimfanya Alie.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY