Straika Wa Pembeni Yanga Kumfuata Mbwana Samata.

Straika Wa Pembeni Yanga Kumfuata Mbwana Samata.

0

Straika Wa Pembeni Yanga Kumfuata Mbwana Samata.

Taarifa zilizo sahihi kutoka ndani ya klabu na mchezaji mwenyewe zinasema Waasland Beveren inayoshiriki ligi kuu ya Ubelgiji iko katika hatua nzuri ya kuweza kumsajili mchezaji huyo.

Straika huyo alijiunga na Yanga akitokea JKU ya Zanzibar ambapo msimu huu amekuwa katika kikosi cha kwanza cha Yanga baada ya kukosekana nyota kadhaa.

Martin anakumbukwa na magoli yake ya mbali msimu 2017-2018 ambayo ameinufaisha timu yake ya Yanga huku ikiwapa nafasi ya mabosi wapya wa Waasland Beveren kumuwinda kwa karibu.

Kwa maelezo ya Emanuel Martin anasema kuwa kila kitu kinaenda sawa kama ikikamilika atakuwa mwenye kuaga Yanga.

“Wiki mbili zilizopita nilipokea simu kutoka kwa mmoja wa mawakala wa nchini Ubelgiji ambaye yeye alipata namba yangu kutoka kwa mmoja wa waandishi wa nchini Rwanda.

“Baada ya kupata namba yangu wakala huyo akanipigia simu na kunipa taarifa hizo ambazo nimezipokea na hivi sasa ninavyoongea na wewe nakamilisha baadhi ya vitu ambavyo ameniagiza na baada ya kukamilisha kaniambia nimpe taarifa,” alisema Martin.

Kama Martin atafanikiwa kukamirisha mipango hiyo ya usajili, basi atakuwa mchezaji wa pili kucheza soka Ubelgiji baada ya Mbwana Samatta anayekipiga Genk.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY