Taarifa Mpya Kutoka Yanga Leo Jumanne.

Taarifa Mpya Kutoka Yanga Leo Jumanne.

0

Taarifa Mpya Kutoka Yanga Leo Jumanne.

Kikosi cha Yanga leo Jumanne ya Juni 26 kinatarajiwa kuanza mazoezi kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya Gor Mahia utakaopigwa nchini Kenya Julai 18.

Viongozi wa klabu ya Yanga Sc wamewaomba wachezaji wao ambao mikataba yao imeisha wajitokeze kwenye mazoezi katika uwanja wa chuo cha Pilisi huku kamati maalumu chini ya Abbas Tarimba ikitafuta pesa kwa ajili ya usajili.

Pia Klabu ya Yanga itatumia mazoezi hayo kuwajaribu baadhi ya wachezaji wa Kimataifa ambao tayari wako nchini wakisubiri kusajiliwa na klabu hiyo.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY