Tetesi za Usajili Barani Ulaya 11 June 2018

Tetesi za Usajili Barani Ulaya 11 June 2018

0

Tetesi za Usajili Barani Ulaya 11 June 2018

Kiungo wa kati wa Lyon na Ufaransa Nabil Fekir, 24, alikuwa na matumaini makubwa kuwa kuhama kwake kwenda Liverpool kungekamilika kiasi kwamba alikuwa tayari amechagua namba ya shati lake. (L’Equipe, via Star)

Kipa wa Roma Alisson, 25, yuko na furaha sana huko Roma licha ya Liverpool kummezea mate kwa mujibu wa kocha wake Claudio Tafferel. (Tele Radio Stereo, via Liverpool Echo)

Mshambuliaji wa Real Madrid na Wales Gareth Bale, 28, atasalia klabu hiyo hadi meneja mpya ateuliwe licha ya Manchester United kuonyesha nia ya kumsaini. (Independent)

 

Paris St-Germain wanataka kumsaini kiungo wa kati wa Chelsea mfaransa N’Golo Kante 27, ambaye ajenti wake amekutana na mkurugenzi wa ligi nambari moja. (Paris United, via Sun)

Arsenal wanakaribia kumaliza kumsaini beki wa Freiburg na Uturuki Caglar Soyuncu , 22, baada ya ajenti wake kuthibitisha kuwa mazungumzo yamefanyika. (Turkish Football, via Sun)

Beki wa Barcelona Joel Lopez, 15, amefikia makubaliano na Arsenal. (Sport)

 

Beki wa Italia Leonardo Bonucci, 31, anasema hana tatizo lolote huko AC Milan baada ya kuhusishwa kwenda Manchester United. (Sky Sport Italia, via Mail)

Real Madrid wanaandaa ofa ya pauni milioni 132 kumnunua kiungo wa kati wa Lazio na Serbia Sergej Milinkovic-Savic.

Mchezaji huyo wa miaka 23 pia anamezewa mate na Manchester United. (Il Messagero, kupitia Express)

Huenda Newcastle wasimwinde mchezaji wa Aston Villa Jack Grealish ambaye thamani yake inawekwa kuwa pauni milioni 30. (Chronicle)

 

Everton, Fulham na Leicester wanamtaka kiungo wa katia wa Norwich na England James Maddison. Mchezaji huyo wa miaka 21 anatajatwa mwenye thamani ya paunia 25. (Northern Echo)

Newcastle inatathmini kumsaini mshambuliaji wa West Brom raia wa Venezuela Salomon Rondon, ambaye mkataba wake una kipengee cha pauni milioni 16. (Northern Echo)

Brighton, Crystal Palace, Southampton na West Brom wameonyesha nia ya kumsaini kiungo wa kati wa Celtic Stuart Armstrong, 26, huku raia huyo wa Scotland akiwa na nia ya kuhamia Premier League. (Record)

 

Wolves wanaandaa ofa kwa kiungo wa kati wa Sunderland na Ireland kaskazini Paddy McNair, 23. (Northern Echo)

Leeds wanaandaa ofa kwa mshambuliaji wa Derby na Jamhuri ya Czech Matej Vydra, 26, ambaye Derby wanataka kumuuza kuweza kupata fedha za kutumia. (Mail)

 

Manchester United, Liverpool na Everton wanamtafuta mshambuliaji wa Wigan Joe Gelhardt, 16, ambaye amekiwakilisha kikosi cha England cha chini ya miaka 16. (ESPN)

Credit : BBC

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY