Tetesi za usajili barani ulaya leo 12 June 2018

Tetesi za usajili barani ulaya leo 12 June 2018

0

Tetesi za usajili barani ulaya leo 12 June 2018

Real Madrid wamewasiliana na meneja wa zamani wa Chelsea na Tottenham Andre Villas-Boas kuchukua mahala pake Zinedine Zidane. (RMC Sport – in French)

Baada ya kuwapata Mauricio Pochettino na Harry Kane kwa mikataba wa muda mrefu, Tottenham wanakaribia kukubaliana mkataba mpya na mchezaji Dele Alli,22, wa thamani ya paunia 100,000 kwa wiki. (London Evening Standard)

Liverpool huenda wasitoe ofa ya kumsaini kipa wa Brazil Alisson, 25, kutoka Roma. (Sky Sports)

 

Alisson anataka hatma yake kutatuliwa kabla ya Brazil kuanza kampeni yake ya Kombe ya Dunia dhidi ya Swizerland siku ya Jumapili. (ESPN)

Kiungo wa kati wa Italia Jorginho, 26, yuko tayari kubaki Napoli lakini kuhamia Manchester City itakuwa fursa ya kihistoria kwa mchezaji huyo kulingana na ajenti wake . (TuttoMercatoWeb via Four Four Two)

Arsenal wako kwenye mazungumzo ya kumsaini kiungo wa kati wa Sampdoria Lucas Torreira, 22, kwa pauni milioni 22 ambaye anaichezea Uruguay kwenye kombe la dunia. (Mail)

 

Fiorentina wameongeza ofa yao ya kumunnua mchezaji wa kimataifa wa Italia Federico Chiesa, 20, hadi pauni milioni 62m – wakati pia anamezewa mate na Liverpool, Manchester City na Manchester United. (Gazzetta dello Sport, via

Meneja wa Jose Mourinho anataka kumsaini mchezaji mmoja zaidi kabla ya Kombe la Dunia na huenda akaanza kumtafuta mlinzi wa Tottenham wa thamani ya pauni milini 50 Toby Alderweireld. (Sun)

Kipa wa England wa kikosi cha chini ya miaka 21 Dean Henderson, 21, ambaye alifikiriwa kulengwa na Arsenal na Chelsea atasaini mkataba mpya na Manchester United.(Mail)

 

Manchester United hawana mipango ya kumsaini mlinzi wa Juventus Mbrazil Alex Sandro, 27, msimu huu lakini wanamtafuta beki mpya wakati fursa iatawadia. (Manchester Evening News)

Liverpool wataweka jitihada za kumsaini kiungo wa kati wa Stoke Xherdan Shaqiri, 26, wakati atarejea kutoka kombe la Dunia. Mirror)

Tottenham wameibuka kama wanaomwinda kiungo wa kati wa Barcelona Rafinha. Mchezaji huyo wa miaka 25 alishinda msimu uliopia huko Inter Milan lakini klabu hiyo ya Italia hawatarajiwi kulipa paunia milioni 30.8 zinazohitajika kumsainia raia huyo wa Brazil kabla ya Juni 30. (Talksport)

 

CSKA wanataka kumuuza mchezaji anayetafuwa na Arsenal Aleksandr Golovin msimu huu lakini watahitaji kwa uchache Euro milioni 25 kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Urusi mweye miaka 22. (Calciomercato)

West Ham ni lazima walipe karibu pauni milioni 7 kummnunu kipa wa Lukasz Fabianski, 33, baada ya ofa yao kukataliwa wiki iliyopita. (Sun)

Mshambuliaji wa Real Madrid na Wales Gareth Bale, 28, atasalia klabu hiyo hadi meneja mpya ateuliwe licha ya Manchester United kuonyesha nia ya kumsaini. (Independent)

 

Kiungo wa kati wa Lyon na Ufaransa Nabil Fekir, 24, alikuwa na matumaini makubwa kuwa kuhama kwake kwenda Liverpool kungekamilika kiasi kwamba alikuwa tayari amechagua namba ya shati lake. (L’Equipe, via Star)

Kipa wa Roma Alisson, 25, yuko na furaha sana huko Roma licha ya Liverpool kummezea mate kwa mujibu wa kocha wake Claudio Tafferel. (Tele Radio Stereo, via Liverpool Echo)

credit : BBC

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY