Tetesi za Usajili Barani Ulaya leo 16 June 2018

Tetesi za Usajili Barani Ulaya leo 16 June 2018

0

Tetesi za Usajili Barani Ulaya leo 16 June 2018

Barcelona imeulizwa kuhusu mshambuliaji wake wa zamani Neymar kurudi katika klabu hiyo. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 aliondoka katika uwanja wa Nou camp ili kujiunga na PSG kwa kitita kilichovunja rekodi cha £200m. (Marca)

Kipa wa Uhispania David de Gea, 27, amekubali mkataba mpya wa miaka mitano na Manchester Uniuted , hatua inayositisha uvumi kwamba huenda akajiunga na Real Madrid. (Manchester Evening News)

 

Paris St-Germain inataka kumsajili kiungo wa kati wa Chelsea na Ufaransa N’Golo Kante. PSG iko tayari kulipa £90m ili kumleta mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 katika klabu hiyo. (Mirror)

Mkufunzi wa klabu ya Nice Patrick Vieira anasema kuwa kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba alionekana kana kwamba amejisahau kama mchezaji soka katika kipindi kirefu cha msimu uliopoita na sasa anahitaji kuimarisha mchezo wake na ‘kutocheza na mashabiki’. (Times – subscription required)

 

Mshambuliaji wa Real Madrid na Wales Gareth Bale, 28, yuko tayari kufanya kazi na kocha mpya wa klabu hiyo Julen Lopetegui badala ya kurudi katika ligi ya Uingereza.. (ESPN)

Real Madrid imekubali mkataba wa kumsaini mshambuliaji wa Santos 17 Rodrygo kwa dau la Yuro 45m-euro (£39.4m) mnamo mwezi Julai 2019. (Guardian)

 

Maurizio Sarri anakaribia kumrithi Antonio Conte kama mkufunzi wa Chelsea. Ajenti Fali Ramadani atazungumza na Napoli wikendi hii ili kujaribu kufikia makubaliano. Sarri bado anahudumia kandarasi yake na klabu hiyo ya Itali hata ijapokuwa tayari mahala pake pamechukuliwa na Carlo Ancelotti. (Independent)

Mchezaji wa zamani wa Chelsea Gianfranco Zola huenda akarudi katika klabu hiyo kama naibu wa Sarri. (sun)

 

Chelsea ina matumaini ya kumzuia kipa wa Ubelgiji Thibaut Courtois, 26. Real Madrid wamekuwa wakimnyatia Courtois lakini sasa wamebadilisha nia yao na wanamtaka kipa wa Roma na Brazil Alisson, 25. (Evening Standard)

Newcastle inakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa Leicester kumsaini winga wa Crystal Palace Andros Townsend. Newcastle iko tayari kulipa £20m kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26. (Guardian)

 

Tottenham inamchunguza kiungo wa kati wa Borussia Dortmund na Ujerumani Mario Gotze. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 huenda akauzwa kwa dau la £16m msimu ujao. (Football.London)

Spurs inakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa Wolves kumsajili kiungo wa kati wa Barcelona na Ureno Andre Gomes, 24. (Sun)

 

Liverpool na Chelsea zinamtaka mchezaji wa Porto raia wa Brazil 25 beki Alex Telles. (Metro via La Parisien)

Wayne Rooney, 32, huenda akaichezea DC United mechi yake ya kwanza mnamo tarehe 14 Julai huku mshambuliaji huyo wa Everton na Uingereza akitarajiwa kuelekea MLS. (Mirror)

Roma inapanga kuiharibia Arsenal kumnunua kipa wa Bayer Leverkusen na Ujerumani Bernd Leno, 26. (Premium via Talksport)

credit : BBC

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY