Tetesi za Usajili barani Ulaya leo 17 June 2018

Tetesi za Usajili barani Ulaya leo 17 June 2018

0

Tetesi za Usajili barani Ulaya leo 17 June 2018

Manchester United itataka dau la pauni milioni 70 kwa ajili ya Anthony Martial 22, ikiwa mfaransa huyo ataendelea kusisitiza kuondoka Old Trafford. (Star on Sunday)

Kutokana nia ya Spurs,Paris St-Germain na Real Madrid,Klabu ya Old Trafford haita mtoa mchezaji wake kwa chini ya pauni milioni 75. (Sunday Mirror)

Maurizio Sarri ameendelea kujiamini kuwa Chelsea itafikia makubaliano na klabu yake ya zamani Napoli ili aweze kuwa Meneja mpya wa Stamford Bridge.(Observer)

 

Real Madrid inataka kumchukua mlinda mlango wa Roma Alisson,kwa kitita cha pauni milioni 50 ambaye pia Liverpool inamuhitaji, lakini klabu hiyo ya Italia inataka kumtoa kwa pauni milioni 75. (Mail on Sunday)

Mshambuliaji Real Madrid Gareth Bale amepata ahueni kwa kuwa meneja wake mpya Julen Lopetegui anaweza kuzungumza kiingereza tofauti na Zinedine Zidane. (Express)

Kiungo wa Arsenal Jack Wilshere,26 anajiandaa kukihama kikosi hicho baada ya kuambiwa kuwa sio sehemu muhimu ya mipango ya Unai Emery. (Sunday Mirror)

 

Southampton iko mbioni kupata saini ya James Maddison wa Norwich City baada ya kukubalika kwa kitita chao cha zaidi ya pauni milioni 20 . (Sun on Sunday)

Mchazaji wa Manchester City Bernardo Silva amesema atajaribu kumshawishi meneja Pep Guardiola kununua wachezaji zaidi kutoka Ureno ili waweze kumsaidia kwenye chumba cha kubadilisha nguo. (The Player’s Tribune)

Huddersfield imeanza mpango wa kumchukua mshambuliaji wa Wolves Ivan Cavaleiro, huku mchezaji huyo akiwa si sehemu ya mipango ya Klabu hiyo. (Mirror)

West Ham imeanza tenza mazungumzo ili kumchukua kiungo wa Paris St-Germain na timu ya taifa ya Argentina, Javier Pastore, 28. (Sky Sports)

Mchezaji wa zamani wa kimataifa Frank Leboeuf anaamini kiungo N’Golo Kante, 27,ni nyenzo muhimu katika matumaini ya Ufaransa kuchukua kombe kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1998. (Standard)

 

Kiungo mshambuliaji wa New Castle Jacob Murphy amerejea kwenye mafunzo ikiwa ni wiki tatu kabla ya msimu kuanza nia ni kujijenga zaidi baada ya kufanya vyema msimu uliopita. (Newcastle Chronicle)

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho amekiri mlinda mlango wake David De Gea, 27 alifanya ”kosa baya ” katika mechi ya kombe la dunia kati ya Uhispania na Ureno lakini amesema” jambo zuri ni kuwa atakuwepo kwenye mechi itakayofuata, hataogopa, akijiamini na kuwa tayari kusaidia timu”.(Sunday Times )

CREDIT : BBC

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY