Tetesi za Usajili barani Ulaya leo 5 June 2018

Tetesi za Usajili barani Ulaya leo 5 June 2018

0

Tetesi za Usajili barani Ulaya leo 5 June 2018

Mshambuliaji wa Liverpool na Senegal Sadio Mane, 26, alikubali kujiunga na Real Madrid kabla ya Zinedine Zidane kujiuzulu kama kocha wa mabingwa hao wa Ulaya. (France Football – in French)

Matumaini ya Chelsea ya kumzuia Eden Hazard yamepigwa jeki na hatua ya Zidane kuondoka Real. Raia huyo wa Ufaransa aliambia mabingwa hao wa Uhispania kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 msimu ujao. (London Evening Standard)

 

Zidane alijiuzulu katika Real Madrid kutokana na mipango ya dirisha la uhamisho la msimu ujao. Klabu hiyo ilikuwa ikitaka kumnunua Kipa wa Manchester United na Uhispania David De Gea 27, lakini Zidane hakutaka. Pia alikasirika kwamba mpango wake wa kutaka kumsajili Hazard haikuungwa mkono. (Sun)

Leicester imefufua hamu yake ya kumsajili mshambuliaji wa Manchester City na raia wa Uingereza Patrick Roberts, 21, ikiwa ni miongoni mwa dau la £60m ambalo litahakikisha kuwa winga wa Algeria Riyad Mahrez, 27, anajiunga na viongozi hao wa ligi. (Daily Telegraph)

 

Mkufunzi wa Tottenham Mauricio Pochettino alikataa kuwa mkufunzi wa Real Madrid kwasababu hakutaka kuonekana kuwa anapenda fedha zaidi. (Daily Mail)

Arsenal inapanga uhamisho wa Marouane Fellaini, 30, ambaye kandarasi yake katika klabu ya Manchester United inakamilika mwezi huu. (Daily Mirror)

Beki wa kulia wa Ureno Diogo Dalot, 19, atafanyiwa uaguzi wa matibabu wiki hii kabla ya kujiunga na klabu hiyo kutoka Porto..(Sky Sports)

 

Sokratis Papastathopoulos anatarajiwa kujiunga na Arsenal kwa dau la £16m kutoka Borussia Dortmund – baada ya beki huyo wa Ugiriki mwenye umri wa miaka 29 kukataa kujiunga na Manchester United, kulingana na babake. (Radio 24/7 via Daily Mirror)

Tottenham haiko katika mazungumzo na Manchester United kuhusu uuzaji wa beki Toby Alderweireld, licha ya madai yanayomuhusisha mchezaji huyo wa Ubelgiji 29 na uhamisho wa kuelekea Old Trafford. (Football.London)

 

Ombi la West Ham la 38m kumnunua kiungo wa kati wa Lazio na Brazil Felipe Anderson, 25, limekataliwa (Gazzetta dello Sport, via Daily Express)

Klabu ya Crystal Palace iko tayari kumuuza Christian Benteke msimu ujao huku hatma ya mchezaji huyo ikiwa haijulikani baada ya kuwachwa nje katika kikosi cha kombe la dunia(London Evening Standard)

 

Leicester inapanga kumnunua mshambuliaji wa klabu ya Uturuki ya Trabzonspor’s Abdulkadir Omur 18. (Leicester Mercury)

Newcastle inataka kumuuza mchezaji wa Senegal Henri Saivet, 27, msimu huu , lakini hamu ya mchezaji huyo ni kuendelea kucheza kwa mkopo (Newcastle Chronicle)

Kinda wa Tottenham Reo Griffiths anatarajiwa kusalia katika klabu hiyo msimu huu. Mchezaji huyo wenye umri wa miaka 17 aliifungia klabu hiyo yenye wachezaji wasiozidi umri wa miaka 18 magoli 30 na alikuwa anapangiwa kuelekea Bundesliga. (London Evening Standard)

 

Mkufunzi wa West Brom Darren Moore anataka kumzuia James Morrison, ambaye kandarasi yake inakamilika mwisho wa msimu huu iwapo kiungo huyo wa kati mwenye umri wa miaka 32 raia wa Uskochi ataonyesha kiwango kizuri cha mchezo wake. (Express and Star)

Bango kubwa la winga wa Manchester City Leroy Sane liliangushwa baada ya nyota huyo mwenye umri wa miaka 22 kuwachwa nje katika kikosi cha kombe la dunia cha Ujerumani. (Daily Mail)

Mmiliki wa Liverpool John W Henry anasema kuwa klabu za ligi ya Uingereza zinafaa kulipwa kitita kikubwa cha mapato ya runinga ughaibuni. (Times)

credit : BBC

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY