Tetesi za Usajili na Sajili zilizokamilika Tanzania 12 June 2018

Tetesi za Usajili na Sajili zilizokamilika Tanzania 12 June 2018

0

Tetesi za Usajili na Sajili zilizokamilika Tanzania 12 June 2018

Hiki ni Kipindi ambacho timu nyingi zimekuwa zikifanya majadiliano na wachezaji mbalimbali mbali na Kuingia nao makubaliano na Kusaini Mikataba ya awali.

AZAM FC WAONGEZA NGUVU

Klabu ya Azam Fc leo msomaji wa Kwataunit.co.ke  imefanikiwa kumnasa nyota wa Njombe Mji Ditraim Nchimbi ambaye amesaini mkataba wa Miaka miwili kucheza Azam Fc msimu Ujao.

MANYIKA HATI HATI KUREJEA SINGIDA

Meneja wa mchezaji Manyika Jr, Mchezaji wa zamani wa Mtibwa Sugar na Yanga Peter Manyika amezungumza na Kusema Kuwa Singida United wamevunja mkaubaliano na Mteja wake Manyika Jr hivyo Hafikirii kama mchezaji huyo atarudi Singida United mpaka watakapomlipa madeni yake yote anayowadai.

ALIYEITIBULIA SIMBA AZIITA TIMU MEZANI

Mchezaji Edward Christopher anaweza kuwa moja kati ya wachezaji wakukum bukwa zaidi msimu huu kutokana na Kufanikiwa kuvuruga sherehe za Simba za Ubingwa kwa Kufunga goli mbele ya Rais wa Nchi ya Tanzania Na Kuharibu rekodi ya Kutofungwa ya Simba.

Mchezaji huyo amefunguka na Kusema amemaliza mkataba wake na kagera na sasa anakaribisha timu yoyote inayomwitaji wafanye mazungumzo.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY