Tetesi za Usajili Yanga leo 26 June 2018

Tetesi za Usajili Yanga leo 26 June 2018

0

Tetesi za Usajili Yanga leo 26 June 2018

Yanga inaendelea na zoezi la Usajili licha ya kuwa wanasisitiza kuwa wanafanya kimya kimya na kila kitu wataweka wazi mara baada ya Kukamilisha zoezi hilo.

Katika nafasi ambazo Yanga wanaonekana kutotaka Kukurupuka ni nafasi ya ushambuliaji na sasa wanahaha kuhakikisha wanapata wachezaji watakaokuwa Mwiba kwa Wapinzani watakapokuwa wanakutana.

Taarifa za Kuaminika  ambazo mtandao wa Kwataunit.co.ke imezipata ni kwamba Yanga wapo katika mazugumzo na Mshambuliaji kutoka Congo Heritier Makambo kutoka katika ligi Kuu ya Congo akicheza katika klabu ya Fc Lupopo.

Mshambuliaji huyo inaelezwa kuwa ni moja kati ya Machaguo ya Kocha Mwinyi Zahera ambaye leo anatarajia kuanza kukinoa Kikosi chake kujiandaa na mchezo wa Kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Gor Mahia.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY