Tetesi za usajili Yanga leo 4 June 2018

Tetesi za usajili Yanga leo 4 June 2018

0

Tetesi za usajili Yanga leo 4 June 2018

Mabingwa wa Kihistoria wa Ligi Kuu soka ya Tanzania Bara Yanga inaelezwa kuwa wapo katika harakati za Kuipata saini ya kipa wa Mtibwa Sugar.

Yanga inaelezwa inapanga Kumrejesha kikosini Benedict Tinnoco ambaye alijiunga na Mtibwa akitokea Yanga na Kutokana na uwezo mkubwa alioonyesha Msimu huu inaelezwa Yanga wapo katika mazungumzo naye.

Inaelezwa pia kwa makipa waliopo kwasasa atabaki kipa mmoja tu ambaye ni Ramadhan Kabwili hivyo ni lazima makipa wengine wawili wasajiliwe ambapo kuna Yule Matampi kutoka Congo na Tinocco huenda akatua Yanga.

INAWEZA KUWA RAHISI TINOCCO KUREJEA YANGA

Kutokana na uhitaji wa Nafasi ya Kipa Yanga ni lazima watatumia kila aina ya ushawishi kumpata kama wanamwitaji lakini pia Tinnoco amemaliza mkataba Mtibwa Sugar na inaelezwa ameaga Mtibwa kuwa hataendelea kuwa nao msimu Ujao.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY