Wachezaji 15 waliobakia kuwania Tuzo mchezaji bora VPL

Wachezaji 15 waliobakia kuwania Tuzo mchezaji bora VPL

0
Wachezaji 15 waliobakia kuwania Tuzo mchezaji bora VPL
Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msimu wa mwaka 2017/2018, ambayo sherehe zake zimepangwa kufanyika Juni 23 mwaka huu.
Wachezaji hao 15 ni miongoni mwa 30 waliotangazwa awali wiki mbili zilizopita kuwania tuzo hizo, ambapo watachujwa kulingana na takwimu mbalimbali za ligi hiyo na kubakia watatu.
Majina ya wachezaji hao watatu yanatarajiwa kutangazwa wiki ijayo, ambapo pamoja na  takwimu ambazo Kamati ya Tuzo inazo, pia itahusisha upigaji wa kura kutoka kwa wahariri wa habari za michezo, manahodha wa timu za Ligi Kuu pamoja na makocha wa timu za Ligi Kuu.
Wachezaji hao 15 na majina ya timu zao katika mabano ni Obrey Chirwa, Papy Tshishimbi na Kelvin Yondani (Yanga),  Shafiq Batambuze, Mudathir Yahya naTafadzwa Kutinyu (Singida United),Wengine ni Adam Salamba (Lipuli), Habibu Kyombo (Mbao), John Bocco, Emmanuel Okwi, Shiza Kichuya na Erasto Nyoni (Simba), Marcel Kaheza (Majimaji), Yahya Zayd (Azam) na Hassan Dilunga (Mtibwa).
Licha ya Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL, pia siku hiyo katika sherehe zitakazofanyika ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam kutatolewa tuzo mbalimbali ikiwemo ya Bingwa wa VPL, Mshindi wa Pili, Mshindi wa Tatu, Mshindi wa Nne na Mfungaji Bora. Tuzo nyingine ni Timu yenye Nidhamu Bora, Mchezaji Bora wa Ligi ya Vijana (Tuzo ya Ismail Khalfan), Mchezaji Bora Chipukizi, Mwamuzi Msaidizi Bora, Mwamuzi Bora,Kipa Bora, Kocha Bora, Goli Bora, Kikosi Bora cha Msimu na Mchezaji wa Heshima.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY