Yanga hawajatoka Kenya bure yaibuka na Winga huyu machachari

Yanga hawajatoka Kenya bure yaibuka na Winga huyu machachari

0

Yanga hawajatoka Kenya bure yaibuka na Winga huyu machachari

Kama ulifikiri Yanga walienda Kenya kwaajili ya michuano ya Sportpesa Supercup pekee basi utakuwa unajidanganya kwani Yanga kwenda na Mwenyekiti wa kamati ya Usajili haikuwa kuuza sura.

Mara baada ya mchezo kati ya Kakamega Homeboys na Yanga mchezo uliomalizika kwa Yanga kufungwa bao 3 kwa 1 Benchi la Ufundi la Yanga na kamati ya Usajili lilivutiwa na Winga mmoja wa Kakamega Homeboys.

Winga Huyo ni Eston Esiye ambaye katika mchezo huo alikuwa msumbufu kwa safu ya Ulinzi ya Yanga, baada ya mchezo kamati ya usajili ya Yanga ikiongozwa na Mwenyekiti wa kamati Hussein Nyika ilichukua mawasiliano na mida ya usiku ikakutana naye hotelini kufanya mazungumzo.

Winga huyo  msomaji wa Kwataunit ukiachana na Kuwa na Kasi nzuri uwanjani pia ni mzuri wa kupiga faulo akikumbukwa may 26 akifunga bao la Mita 35 kwa Free Kick wakati Kakamega ikiangamiza Tusker bao 2 kwa 0.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY