Achana na Nduda mchezaji mwingine ajiondoa Simba Kimyakimya

Achana na Nduda mchezaji mwingine ajiondoa Simba Kimyakimya

0
Emmanuel Mseja atoweka Simba

Achana na Nduda mchezaji mwingine ajiondoa Simba Kimyakimya

Wakati Simba ikiwa inaendelea na matayarisho kwaajili ya mchezo wa Robo Fainali ya Kagame Cup 2018 kesho awali iliripotiwa kuwa kipa Said Mohammed “Nduda” amegoma kufanya mazoezi na timu hiyo kutokana na kukosa nafasi lakini pia kutoridhishwa na mambo yanayoendelea Simba.

Lakini Taarifa nyingine ambazo kwataunit.co.ke Imezipata ni kuhusu Kipa namba tatu wa Simba Emmanuel Mseja kujiondoa kimya Kimya kwenye Kikosi cha Simba sababu zikielezwa kuwa ni kutokana na kusikia tetesi kuwa Simba hawana Mpango naye kwaajili ya Msimu Ujao baada ya Mkataba wake Kuisha.

Kipa huyo amekuwa hapati nafasi ya Kucheza akimaliza msimu uliopita bila Kucheza hata mechi moja ya Ligi Kuu badala yake alicheza michezo ya MapinduzI Cup pekee na sasa hali imezidi kuwa ya Mashaka kwa Upande wake kwani  ameongezeka Kipa Mwingine Dida huku Kinda Ally Salim akionekana kuaminiwa na Kocha Masoud Djuma.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY