Alichosema Pierre Kwizera baada ya Kuhusishwa kusaini Yanga

Alichosema Pierre Kwizera baada ya Kuhusishwa kusaini Yanga

0

Alichosema Pierre Kwizera baada ya Kuhusishwa kusaini Yanga

Yanga imekuwa ikihusishwa kuhitaji wachezaji wengi msimu huu lakini siku mbili tatu hizi imekuwa ikitajwa Kutua mpaka kwa Kiungo Mburundi anayecheza Rayon Sports ya Rwanda Pierre Kwizera.

Pierre Kwizera amekuwa akitajwa kuwa kwenye rada za Yanga huku taarifa zaidi zikisema ameshakubaliana na Yanga na huenda akasaini mkataba wa Miaka miwili Yanga.

Habari Njema Kutoka Yanga leo Jioni

Kiungo huyo akizungumza na EFM leo amefunguka kuwa hakuna chochote kinachoendelea kati yake na Yanga kwani hakuna Kiongozi yoyote wa Yanga ambaye ameshazungumza naye.

“Taarifa za Kusema mimi natafutwa na Yanga bado ni maneno tu, hakuna kiongozi wa yanga ambaye ameshanifata nikafanya naye mazungumzo. “

Akizungumzia kuhusu Kusaini Miaka 2 Yanga amefunguka

” Wanasema nimeshasaini miaka miwili bado sijasaini nina mkataba na Rayon Sports utaisha mwisho wa MWEZI Huu, kukiwa kuna taarifa za mimi kwenda Yanga nitawajulisha “

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY