Baada ya Mo Banka,Yanga inatajwa kuwa Mbioni Kumtangaza mchezaji huyu

Baada ya Mo Banka,Yanga inatajwa kuwa Mbioni Kumtangaza mchezaji huyu

0

Baada ya Mo Banka,Yanga inatajwa kuwa Mbioni Kumtangaza mchezaji huyu

Baada ya kumpa kandarasi ya Miaka 2 mchezaji Mohammed Issa maarufu zaidi kama Mo Banka kutoka Mtibwa Sugar inaelezwa Yanga ipo mbioni kumsainisha Msauzi.

Msauzi huyo ni Masete Kingslay Makgatho ambaye alitua nchini kwaajili ya majaribio na sasa inaelezwa mambo yake mazoezini yamekuwa moto kiasi cha kumvutia Kocha Mwinyi Zahera.

AKISAJILIWA HUYU ANAACHWA.

Taarifa kutoka chanzo cha kuaminika zinaeleza kuwa kama Masete Kingslay Makgatho atasainiwa Yanga basi itakuwa inaachana rasmi na kiungo wake Thaban Kamusoko.

Kamusoko inaelezwa kuwa amekuwa haonekani mazoezini Yanga lakini pia majeraha na Umri vinawafanya Yanga kuamua kutafuta mbadala wake mapema.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY