Cannavaro Atema Nyongo Yanga  Kuhusu Mishahara

Cannavaro Atema Nyongo Yanga  Kuhusu Mishahara

0

Cannavaro Atema Nyongo Yanga  Kuhusu Mishahara

Nahodha wa klabu ya Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ amesema hatoweza kamwe kuendelea kuichezea timu yake hata kama tatizo la uhaba wa fedha litaendelea kuiandama.

Beki huyo aliyeichezea Yanga kwa mafanikio na muda mrefu, ameeleza klabu hiyo imemtoa mbali zaidi hivyo ataendelea kuitumikia mpaka pale umri wake utakapokuwa umemshika mkono.

Kauli ya Cannavaro imekuja kufuatia baadhi ya wachezaji wa Yanga kuanzisha migomo baridi hivi karibuni kutokana na madai ya mishahara huku wengine wakiondoka na kuelekea mahala pengine.

Lakini Nahodha huyo wa muda mrefu, ameamua kufunga na kuelezea hisia zake ndani ya Yanga ambayo imemtoa mbali akisema hawezi kuiacha kwa namna yoyote ile.

Kikosi cha Yanga kipo katika maandalizi ya kikijiandaa na mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Gor Mahia FC utakaopigwa Kenya Julai 18 2018 kwenye Uwanja wa Machakos jijini Nairobi.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY