Dili la Kocha Mpya Simba, Mbona Mambo Ni Hivi!

Dili la Kocha Mpya Simba, Mbona Mambo Ni Hivi!

0

Dili la Kocha Mpya Simba, Mbona Mambo Ni Hivi!

Unapozungumzia taarifa zinazobamba mtaani basi huwezi kuiacha hii ya kocha mpya wa Simba, Ukiachilia mbali mshangao ambao viongozi wa Simba waliuacha kwa mashabiki fahamu ya ziada kuhusu usajili wa kocha huyo..

Kocha huyo aliyewahi kuwanoa mabingwa wa Kombe la Shirikisho Afrika, AC Leopards ya Congo Brazzaville ametua nchini tangu Jumapili na amezishuhudia mechi mbili za Simba katika Michuano ya Kombe la Kagame na sasa anasubiri kusaini tu.

Habari za uhakika kutoka ndani ya Kamati ya Usajili ya Simba zilisema Aussems ametua hapa nchini ili kusailiwa baada ya kuwavutia mabosi wa Msimbazi kwa CV yake ya kutisha miongoni ma makocha kadhaa walioomba kazi ya kumrithi Pierre Lechantre.

“Nikwambie tu, Aussems amekuja kusailiwa na kwa sasa tunajadili naye kuweka mambo sawa kabla hajasaini. Mipango yetu ni kumpa mkataba wa mwaka mmoja tu kwanza kisha mbeleni ndipo tutauongeza,” alidokeza mmoja wa vigogo hao wa Simba aliyeomba kuhifadhiwa jina.

“Unajua tumepokea maombi ya makocha wengi ikiwemo Muingereza Johnny McKinstry, wote wakitaka kuchukua nafasi ya Mfaransa, lakini Mbelgiji aliwafunika

wenzake kwa rekodi za soka la Afrika ndio maana tulimuita aje tumsaili.”

“Asilimia kubwa mambo yamekwenda vizuri na mpaka tumefika hatua ya kukaa chini na kufanya mahojiano nae tumeona ana nafasi kubwa ya kufanya kazi Simba,” alisisitiza.

Naye Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa Simba, Said Tulliy alisema mambo yote ya kutafuta kocha yanaenda sawa, ila hawatamtangaza hadi Michuano ya Kagame imalizike.

“Tunatengeneza timu kwa kufanya usajili katika maeneo yenye upungufu, lakini pia ni lazima tuwe na kocha anayeweza kutufikisha pale Simba inapopataka, ila subiri mtatangaziwa ni nani atamrithi Lechantre baada ya Kagame.”

Naye Mjumbe wa Kamati ya Mabadiliko ya Simba, Mulamu Ng’hambi alisema klabu yao ipo kwenye mchakato wa mabadiliko yatakayoifanya iwe timu kubwa na bora ndio maana kila kitu chao kinafanywa kwa umakini mkubwa na usiri.

“Sifahamu kocha gani atakuja kuifundisha Simba, ila ninachofahamu wanatafuta yule atakayelifahamu vizuri soka la Afrika kwa kufanya vizuri huko alipotoka,” alisema.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY