Habari njema kutoka Yanga asubuhi Hii 31.7.2018

Habari njema kutoka Yanga asubuhi Hii 31.7.2018

0

Habari njema kutoka Yanga asubuhi Hii 31.7.2018

Klabu ya Yanga mapema  mwezi wa tano ilielezwa kumalizana kila kitu na Kocha raia wa Congo Mwinyi Zahera na kusaini naye mkataba wa miaka miwili kama kocha mkuu wa Klabu ya Yanga.

Lakini kocha huyo toka aliposaini Yanga ameshindwa kusimama katika benchi kama kocha mkuu wa timu katika mechi zote ambazo Yanga imekuwa ikicheza wakati yeye ndiye kocha Mkuu.

Sababu kubwa iliyokuwa inaelezwa kusababisha tatizo hilo ni kukosekana kwa vibali vya kazi vya kocha huyo kuruhusiwa kufanya kazi.

Mwenyekiti wa kamati ya mashindano Hussein Nyika amethibitisha kuwa jana vibali vya kocha Mwinyi Zahera vilikamilika na vingekamilika toka wiki iliyopita lakini kuna mambo yalikwama Ijumaa, Kwahiyo kwasasa kocha huyo ni ruksa kusimama kwenye benchi Yanga itakapocheza mechi zake.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY